Lakini wamesahau ya kwamba maisha yao na mafanikio yao wameyabeba wenyewe na wala si serikali, marafiki, familia, ndugu kutaja wachache.
Leo nimechagua msemo huu wa "Pambana na hali yako" kwa sababu umebeba funzo kubwa ambalo tunahitaji kulifahamu.
Je kupambana na hali yako ni nini?.
Hii ni hali ya kujisemesha mwenyewe na kuhamua liwalo na liwe lazima nifanikiwe bila kutegemea msaada wa mtu mwingine.
Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu dunia ya Leo imebadilika, kila mtu anawaza namna ya kuweza kufanikiwa kwenye maisha yake binafsi ndiyo maana muda mwingi anajikuta akijiendeleza yeye binafsi. Ndio maana nikasema pambana na hali yako.
Kila siku hakikisha unafanya kitu kitakachokusaidia kujikwamua na kutoka mahali ulipo kusogea hatua Fulani. Nakubaliana na Martin Luther King Jr aliyewahi kusema " kama huwezi kupaa, kimbia. Kama huwezi kukimbia, tembea. Kama huwezi kutembea, tambaa. Kwa njia yoyote hile hakikisha unasogea hatua Fulani."
Hivyo ndivyo maisha yako ya kila siku unatakiwa huyajenge. Hakuna mtu atakayekuja kukupeleka wewe kwenye mafanikio unayoyataka kama wewe haupo tayari kuweka juhudi kuyatafuta mafanikio yako mwenyewe, pambana na hali yako.
Mwanafunzi usitegemee mwalimu akufundishe kila kitu, jisomee wewe mwenyewe tafuta maarifa zaidi ya kile alichokitoa mwalimu darasani. Usiishie kusema yaani mwalimu yale mambo hakufundisha, pambana na hali yako.
Mkulima unaweza kulalamika mvua hazinyeshi, wakati watu wa Misri wanaishi katika nchi kame, lakini bado wanaongoza kwa kulima matunda. Wewe mkulima acha kulalamika, kuna kilimo cha umwagiliaji, pambana na hali yako.
Mfanyabiashara, unaweza kuwa unalalamika haupati wateja, kumpe tatizo linaanzia hapo dukani kwako, waajiri wako hauwahudumii vizuri, huwapendi, unategemea watawahudumia wateja wako vizuri?, unachelewa kufungua biashara yako na unawahi kufunga, unafikiri hapo kweli utapata wateja? hapana tena HAPANA kubwa, pambana na hali yako.
Kila mtu katika sehemu aliyopo akiweza kupambana na hali yake, tunaweza kuona mabadiliko makubwa na mafanikio makubwa pia.
Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako makala hii ili naye ajifunze.
Jipatie kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio kwa bei ya shilingi 6000/=
2 comments:
Great one
Sawa iko Poaa... Ujumbe mzuri
Post a Comment