Saturday, 29 July 2017

Kitu Unachopaswa Kuwa Nacho Kabla Ya Kuanza Biashara Yoyote

Watu wengi, wamekuwa wanawaza sana kuanza kufanya biashara kila kukicha. Wapo watu wengi wenye mawazo mengi na mazuri ambayo yanaweza kuyatajirisha.
Ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa haraka sana kiuchumi lazima uuze. Kila aliyefanikiwa kiuchumi lazima kuna kitu ambacho anakiuza.

Leo nataka nikwambie kitu kimoja muhimu sana unachohitaji kabla ya kuanza kufanya biashara yoyote.


Kitu ambacho nataka nikizungumzie Leo ni uaminifu. Uaminifu ni cha muhimu sana ambacho kila mfanyabiashara au mjasiriamali yoyote anapaswa kukijenga kabla ya kuanza kufanya biashara.

Kama watu hawakuamini biashara yako inaweza kufa punde tu hata baada ya mwezi mmoja kuanzishwa. Wateja wako inabidi wawe watu wanaokuamini, kama watu hawana imani na wewe sio rahisi kufanya biashara na wewe.

Anza Leo kujenga uaminifu kwa watu wanaokuzunguka kwenye mazingira yako maana biashara yoyote lazima ianzie kwenye mazingira yanayokuzunguka. Watu wanaokuzunguka ndio wateja wa kwanza wa biashara utakayoianzisha. Huwezi kuwaza kuuza bidhaa yako kwa watu wa mbali wakati umeshindwa kuwauzia watu wa karibu. Marafiki zako na ndugu zako wawe watu wanaokuamini. Kama ukienda kukopa kwa marafiki zako pesa ya kuanzisha biashara yako na marafiki zako wote hata ndugu zako akakosa hata mtu mmoja wa kukukopesha tambua kwamba watu hao hawakuamini. Na kama marafiki zako wa karibu na hata watu wa familia yako hawakuamini ni bora usitishe biashara unayotaka kuianza.

Unaweza kuwa huna mtaji wa kuanza biashara lakini kuna watu wengi wenye pesa ambazo hawazitumii kama wamejenga uaminifu juu yako wanaweza kukupatia pesa zao uanze nazo kama mtaji.

Kumbuka; Jenga uaminifu kabla ya kuwaza kuanzisha biashara yako.

"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako makala hii ili naye ajifunze.

Jipatie kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio kwa bei ya shilingi 6000/=



Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: