Sunday, 15 January 2017

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeiona siku ya Leo salama kabisa.

Karibu sana katika mada ya Leo "Fungua Moyo"
Kufungua moyo ni kuwa tayari kukabiliana na jambo lolote.

Nilipokuwa Jeshi kwa mujibu wa sheria Msange JKT Tabora, neno hili lilitumika kutuasa vijana kupokea mafunzo ya kijeshi kwa moyo wote.

Kufungua moyo ni kujitoa kwa moyo wote katika kufanya kile unachoitaji. Hili ufanikiwe lazima na wewe ufungue moyo. Nafikiri kati ya maneno yanayomsaidia na kumuhamasisha mwanajeshi katika mafunzo yake ni neno "fungua moyo".

Kama ni mwanafunzi unahitaji kufungua moyo. Kama ni mfanyabiashara unahitaji kufungua moyo. Kama ni mfanyakazi unahitaji kufungua moyo na kuipokea kwa amasa kazi unayoifanya.

Kufungua moyo kunaondoa uoga wa kile unachokifanya kwa kuwa na utayari ndani mwako.

"Mtu ambaye hajawahi king'atwa na nyoka siku zote umuogopa jongoo" ni methali ya watu wa Ghana.

Ukifungua moyo utakuwa tayari kukabiliana na jambo lolote, hata kama kuna milima kwenye maisha yako wewe utaona mabonde. "Njia hutengenezwa kwa kutembea" ni methali ya Kiafrika.
Kama ni mwanafunzi kufungua moyo ni kujitoa na kusoma kwa bidii. Kama ni mfanyabiashara kufungua moyo kufungua moyo kwako ni kutambua kwamba unahitaji kutoa huduma iliyo bora na pia kuna kushuka na kupanda yaani katika biashara kuna faida na hasara. Hata kama umeoa au kuolewa unahitaji kufungua moyo pia, kufungua moyo kwako ni kutambua yakwamba mwenza wako sio mkamilifu ana mapungufu ya hapa na pale kwani duniani hakuna mtu aliyekamilika. Kama ni kazi kufungua kwako moyo ni kuamka asubuhi na mapema kwenda kazini na pia kufanya kazi kwa bidii.

Kufungua moyo ni kujifunza, ukiwa umefungua moyo itakuwa tayari kuyapokea Yale yote unayoelekezwa na wakubwa zako kwani "kuku mkubwa ufundisha kifaranga".

Je wewe umefungua moyo kwa kile unachokifanya?.
Leo nakusihi fungua moyo ufanikiwe.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Bide Katamugora

Tuwasiliane:
0764145476.
Whatsapp:0625951842 ( tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
Email: ekatamugora@gmail.com

Usisite kuwashirikisha na wenzio kile unachokipata.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: