Mitandao ya kijamii imeteka kwa kiasi
kikubwa biashara nyingi hii ni kwasababu watu wengi wanatumia mitandao ya
kijamii. Na moja wapo ya kanuni za kufanya mauzo ni kuwafata wateja mahali
walipo. Wateja wengi wapo kwenye mitandao ya kijamii hivyo ni wajibu wako
kuwafata huko.
Wakati watu wengine wanajiunga na
mitandao ya kijamii ili waweke picha zao na maandishi ya kuchekesha kusudi
wapate like kuna watu wengine
wametengeneza pesa kubwa kupitia mitandao ya kijamii. Je wewe umewahi kufikiri
kutengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii?
FAIDA
ZA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII
1. Ni rahisi sana
kujifunza hivyo mtu yeyote anaweza kujifunza na kuanza kuitumia mitandao ya
kijamii kikamilifu.
2. Ni gharama
ndogo ya kujitangaza kwa wateja ukilinganisha na magazeti na TV.
3. Mitandao ya
kijamii hujenga uaminifu. Watu wanapenda kufanya biashara na mtu wanayemfahamu.
Hivyo ni rahisi kupata wateja wanaokufatilia kwenye mitandao yako.
4. Unaweza kuwasiliana
na wateja wako moja kwa moja.
5. Mitandao ya
kijamii itakusaidia kupata wasomaji wa blogu au website yako kama unamiliki
blogu au website.
6. Mitandao ya
kijamii itakusaidia kujua na kufanya uchunguzi wa soko. Utajua watu wanataka
nini na hawataki nini.
7. Inakuongezea uthamani.
Ukiweza kuwa mtu anayeweka mambo ya maana kwenye mitandao yako, thamani yako
itapanda.
8. Watu watakutafuta
na kufanya kazi na wewe. Ukitengeneza jina lako vizuri katika mitandao ya
kijamii watu wakubwa watahitaji kufanya kazi na wewe. Mimi ni shuhuda wa hili,
baada ya kuanza kuandika Makala mbalimbali katika blogu yangu ya BIDEISM
nimekuwa nikitafutwa na watu mbalimbali ili tufanye kazi pamoja.
9. Itakufungulia connection
mpya. Ukiweza kujibrand vizuri utaweza kufanya kazi na kupata connection kubwa
ambazo hata kabla ulikuwa huzitarajii.
JINSI YA KUTENGENEZA BRAND YAKO MTANDAONI.
1.
Hakikisha
unaandika mambo yanayowagusa watu mara nyingi uwezavyo. Kuna watu wengi
wanatafuta namna ya kutatua matatizo yao. Ni jukumu lako kuwaonesha namna gani
wanaweza kuyatatua. Hii itakuchukua muda watu kuanza kukuelewa na muda mfupi ambao utakuchukua ni miezi 6. Watu
mara nyingi sio rahisi kukuelewa lakini kadri unavyoendelea watakuelewa. Hivyo usikate
tamaa.
2.
Angalia
wenzako wanafanya nini katika mitandao yao ya kijamii. Ukiona kuna mtu anafanya
kitu ambacho ulikua ukitamani kukifanya mtafute na ikiwezakana omba ushauri
kwake akupe njia yeye anawezaje. Kama yeye ameweza unaweza pia. Kama mimi
nimeweza, wewe pia unaweza.
3.
Kuwa
mtu wa watu. Ukiwajali watu watakujali pia. Unahitaji kuwa mtu wa watu katika
mitandao ya kijamii. Wajibu watu kwa heshima, tumia maneno kama; kaka au dada
yanasidia sana. Asikwambie mtu watu wanapendwa kuheshimiwa. Ukiwapa heshima
watakuja kwako.
4.
Uonesha
ujuzi wako:
Kuna
watu wengi wana ujuzi lakini kwenye mitandao yao ya kijamii hawoneshi ujuzi
huo. Wanafanana na yule mtu aliyepewa talanta akaificha. Usikubali kuwa na
ujuzi halafu kwenye mitandao yako ya kijamii hauuoneshi. Ujuzi wako ni pesa
uliyoikalia.
JINSI YA
KUJITANGAZA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII
Takwimu zifuatazo zinaonesha matumizi ya mitandao
ya kijamii nchini Tanzania toka Machi 2017 hadi mwezi Machi 2018:
MTANDAO
|
ASILIMIA YA WATUMIAJI
|
Facebook
|
59.98%
|
Youtube
|
17.36%
|
Pinterest
|
12.67%
|
Twitter
|
5.97%
|
Instagram
|
2.27%
|
Google+
|
0.67%
|
Ukichunguza
kwa ukaribu unaweza kujua ni mtandao upi ambao una watumiaji wengi. Unahitaji pia
kujua wateja wako wanatumia mtandao upi na inakupasa ujiunge pia na mtandao
huu. Kumbuka biashara huenda kule wateja waliko. Kama wateja wako wanapatikana
WhatsApp hakikisha umejiunga Na WhatsApp pia.
MAMBO YA KUFAHAMU KABLA KUANZA KUTUMIA MITANDAO YA
KIJAMII KUJITANGAZA:
· MALENGO:
Unahitaji
kuanza kwa kuandika malengo yako kwanini unataka kutumia mitandao ya kijamii
kujibrand na kufanya biashara. Hatupangi kushindwa tunashindwa kupanga, watu
wengi hawapangi ndiyo maana malengo yao hayatimii.
· Jua ni wapi
wateja wako. Ukijua watu gani watakua wateja wako utakua umejiweka kwenye
wakati mzuri. Je ni vijana? wazee Au wanafunzi, wazazi, kutaja wachache.
· Ni wapi
wanapatikana.
Ukijua
ni mitandao gani wateja wako wanapatikana hakikisha unawafata huku. Hapo utakuwa
umelishika soko lako.
MAMBO YA KUZINGATIA:
1.
Uaminifu.
Kama
hautakuwa mwaminifu katika kazi zako ni bora usifanye biashara kupitia mitandao
ya kijamii. Uaminifu ni nguzo kubwa katika kufanya biashara kupitia mitandao.
2.
Kanuni
ya 7/1
Kama
katika post unazoziweka katika mitandao yako ya kijamii hakikisha post 6
zinazungumzia au kuelezea bidhaa zako na ujuzi wako na post moja ambayo ni ya
saba ndiyo iwe tangazo la bidhaa yako. Ukiwa mtu wa kutangaza bidhaa tu
utawaboa watu na wataacha kukufatilia. Weka vitu vingi vinavyowaelimisha na
ndipo uweke matangazo ya bidhaa zako.
3.
Kuwa
muwazi.
Ukionekana
kwenye mitandao ya kijamii onekena kama mtaalamu. Usionekane kama watu wengine.
Kumbuka watu wanhukumu kava ya kitabu na ni kilicho ndani ya kitabu.
4.
Unahitaji
kuwa mbunifu. Usifanye mambo kwa mazoea, kila siku jiulize swali ili:
nitafanyaje kwa ubora zaidi ya jana? Hilo ni swali unalopaswa kujiuliza kila
siku.
UZUSHI KUHUSU
MITANDAO YA KIJAMII
Kuna
uzushi mwingi utausikia lakini na kuahakikishia kwamba mitandao ya kijamii ni
chaguo jema kama utakua kweli umeamua kijutanua kibiashara.
Uzushi kwamba
mitandao ya kijamii ni ya watoto:
Utasikia
kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa na watoto lakini jambo hilo sio la kweli
kabisa. Takwimu zinaonesha kuwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 35 ndiyo
wamekuwa watumiaji wakubwa wa mtandao wa Facebook, umri kuanzia miaka 24 hadi
34 huongezeka mara mbili kila baada ya miezi sita. Watu wengi wanaotumia
mtandao wa Twitter wana umri wa miaka 35-49. Watumiaji wa mtandao wa LinkidIn
wanao wastani wa umri wa miaka 41.
Uzushi kuwa
unahitaji utaalamu wa teknolojia kutumia mitandao ya kijamii:
Kwenye
matumizi ya mitandao ya kijamii hauhitaji kuijua sana teknolojia ndipo uanze
kuitumia. Kanuni ya 80/20 inasema 80% ya unachokiweka mtandaoni ni kile
unachokitoa na 20% ni ujuzi wa teknolojia. Hivyo usiogope kuhusu teknolojia.
Najua
umefunguka sana kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii. Usisoke kusoma Makala zinazofuata
kwenye blogu hii. chini kabisa ya blogu hii unaweza kudownload APP ya blogu hii
ili upate Makala zinazofuata ili kujifunza Zaidi. Bofya sehemu iliyoandikwa
DOWNLOAD OUR APP chini kabisa ya ukurasa huu ili upate APP yetu bure.
Mafanikio Yako
Mikononi Mwako.
Ndimi:
EDIUS
KATAMUGORA
0764145476
Washirikishe
na wenzako Makala hii. Mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
0 comments:
Post a Comment