Tarehe 5, mwezi oktoba mwaka huu nilitumiwa meseji (SMS) na mojawapo ya wasomaji wangu akisema:
"Habari, samahani naitwa Eliada nipo Arusha ni mwanafunzi nipo certificate nasomea utangazaji.
Ninashida kaka nikiwa studio nashikwa na hofu na uoga hadi nashindwa yaani sijiamini naomba unielekeze.
Shida yangu kubwa ni confidence ya kuongea studio nikishafika studio tu pakiwa na watu siwezi kuongea naogopa."
Kwanza kabisa niseme hofu ya kuongea mbele za watu huwakumba watu wengi lakini ni kitu cha kujifunza kama unavyojifunza masomo ya darasani.
( Nikiongea na wanafunzi wa Kahororo na Nyakato Highschools)
Sisi watu ambao tunajishughulisha na mambo ya kuongea hadharani(public speaking) huwa tunashauriwa mambo 3 hili tuweze kuondoa hofu ya kuongea mbele ya watu.
Lakini kila mtu anaweza kuzitumia hili kuua kabisa ugonjwa huu unaowasumbua wengi. Kama ukiwa na hofu ya kuongea mbele za watu ni wazi kwamba kufanikiwa kwako kutakuwa kwa kusuasua.
Katika karne ya ishirini na moja kitu kikubwa kinachohitajika kwenye biashara ni mawasiliano sasa kama una hofu ya kuongea mbele ya watu huwezi kufanya biashara. Na ili mtu awe na uhuru wa kiuchumi lazima afanye biashara na kuwekeza katika maeneo mbalimbali.
Vitu 3 unavyovihitaji ili kuondoa hofu ya kuongea mbele ya watu:
1) Andaa kile utakachoongea:
Watu wengi hushindwa kuongea mbele za watu kwasababu tu hajiandai ipasavyo kuongea mbele ya watu.
Watu wengi hushindwa kuongea mbele za watu kwasababu tu hajiandai ipasavyo kuongea mbele ya watu.
Mfano mwanafunzi kama anawasilisha mada Fulani (presentation) mbele ya wanafunzi wenzake, kama hakujiandaa lazima atashindwa kuongea mbele ya wanafunzi wenzake hii itamletea hofu ya kusema hili silijui itakuaje nikiulizwa swali la sehemu ambayo sijaipitia. Hofu huanzia hapo. Hivyo jambo la kwanza kabisa la kuua hofu ni kujitahidi kujiandaa ipasavyo kabla ya kuongea mbele ya watu.
2) Amini katika kile unachokiongea.
Kujiandaa haitoshi kama hauamini katika kile unachokiongea mbele ya watu. Kutoamini kile unachokiongea huleta wasiwasi mkubwa na hatimaye mtu hushikwa na hofu ya kuongea mbele ya watu akijua labda watu anaaongea nao kuna mtu anajua zaidi yake hivyo lazima tu atashindwa kuongea mbele ya watu.
Kujiandaa haitoshi kama hauamini katika kile unachokiongea mbele ya watu. Kutoamini kile unachokiongea huleta wasiwasi mkubwa na hatimaye mtu hushikwa na hofu ya kuongea mbele ya watu akijua labda watu anaaongea nao kuna mtu anajua zaidi yake hivyo lazima tu atashindwa kuongea mbele ya watu.
Mfano sisi tulio katika sekta ya uhamasishaji tunashauriwa kutokubali mialiko ya kuongealea mambo ambayo hatuyafahamu kwa undani. Hata kama unalipwa pesa kubwa kiasi gani.
Mfano ukinihitaji niende kuongea na wakulima siwezi kufanya vizuri kama atakavyofanya ndugu yangu Joseph Mwakyoma ambaye ni mtaalamu wa mambo ya kilimo.
3) Fanya mazoezi;
Kama nilivyotangulia kusema, kuongea mbele za watu ni ujuzi ambao unafundishika. Hivyo ni jambo linalotakiwa kufanyiwa mazoezi Mara kwa mara.
Kama nilivyotangulia kusema, kuongea mbele za watu ni ujuzi ambao unafundishika. Hivyo ni jambo linalotakiwa kufanyiwa mazoezi Mara kwa mara.
Wataalamu wa Neurolojia wanasema "Ili mtu awe amebobea katika fani flani anaitaji masaa 10000 ya kufanya mazoezi katika fani yake, awe mwanamuziki, mwandishi, mhamasishaji, mcheza mpira, na hata jambazi sugu."
Sasa kuweza kupata hayo masaa 10000 lazima hujitahidi kufanya mazoezi ya kuongea mbele za watu mara nyingi kadri uwezavyo.
Aristotle mwanafalsafa wa zamani aliwahi kusema, "Ukitaka kujifunza kucheza zumari, sharti ucheze zumari." Kumbe Ukitaka kuongea bila uoga mbele ya watu sharti uongee mbele za watu.
Unaweza kufanya mambo yafuatayo kama kufanya mazoezi ya kuongea mbele ya watu.
1) Kila siku chukua kitabu nenda mbele ya kioo na soma kurasa zisizopungua 20 kwa sauti kubwa. Ukiweza kuongea bila kusoma kitabu itakuwa vyema pia na itakuondolea hofu.
2) Jenga picha:
Jenga picha ukiwa unajiona unaongea mbele ya watu. Kujenga picha husaidia hata katika kujiona unakuaje. Fikiria unaongea na kikundi cha watu 200.
Jenga picha ukiwa unajiona unaongea mbele ya watu. Kujenga picha husaidia hata katika kujiona unakuaje. Fikiria unaongea na kikundi cha watu 200.
Winston Churchill (30, Novemba 1874- 24 Januari 1965) aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza aliwahi kusikika akitoa hotuba akiwa bafuni anaoga. Fikiria kiongozi mkubwa kama huyu anafanya mazoezi bafuni!.
3) Anza na kuongea katika vikundi vidogo vidogo vya watu.
Wachina wanasema "Safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja." Hivyo ili kuongea mbele za watu wengi anza kuongea na watu wachache wachache. Kama ni watu watano hakikisha umechangia lolote au unaendesha mjadala. Wahenga walisema "Hata mbuyu ulianza kama mchicha."
Vitu viwili vya ziada unavyovihitaji unapoongea mbele za watu:
1) Mavazi yako:
Wazungu husema "First impression matters." Wakimaanisha "Namna unavyoonekana mbele ya watu inasaidia." Watu wanaweza kukuhukumu kutokana na mavazi unayovaa au ukiyovaa. Hakikisha unapokwenda kuongea mbele ya watu unavyaa kitanashati. Les Brown mhamasishaji wa Kimarekani aliwahi kusema "Vaa kama mtarajiwa, usivae kama mtuhumiwa."
Wazungu husema "First impression matters." Wakimaanisha "Namna unavyoonekana mbele ya watu inasaidia." Watu wanaweza kukuhukumu kutokana na mavazi unayovaa au ukiyovaa. Hakikisha unapokwenda kuongea mbele ya watu unavyaa kitanashati. Les Brown mhamasishaji wa Kimarekani aliwahi kusema "Vaa kama mtarajiwa, usivae kama mtuhumiwa."
Kitu kizuri zaidi kama umevaa mavazi ya heshima hutokuwa na hofu ya watu watanionaje na hapo ndipo hofu ya kuongea mbele za watu huanzia.
2) Matendo ya mwili:
Maneno unayozungumza huchukua asilimia 35 tu ya kile unachokiongea lakini matendo yako ya mwili (body language) huchukua asilimia 65, wengine wamekwenda zaidi na kusema 70%.
Maneno unayozungumza huchukua asilimia 35 tu ya kile unachokiongea lakini matendo yako ya mwili (body language) huchukua asilimia 65, wengine wamekwenda zaidi na kusema 70%.
Ukitaka kujifunza matendo ya mwili angalia watu mashuhuri unaowakubali wakiwa wanaongea mbele za watu miili yao inakuaje. Angalia mienendo ya mikono yao, hapa kuna lugha ya kujifunga na kujifungua (open and closed language), mfano mtu anayeongea amefunga mikono yake kama yupo kanisani akisali hawezi kupokelewa vizuri na watu (hii huitwa lugha ya kujifunga) lakini anayeongea akipeleka mikono yake sehemu mbalimbali ni rahisi kuwakamata wale anaoogea nao.
Mfano ingia katika YouTube angalia mtu anayeitwa Vusi Thembekwayo anavyoongea mbele za watu utajifunza mengi kuhusu matendo ya mwili.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu kwa namba 0764145476. Tunatuma mikoa yote.
Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza kwani mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
2 comments:
Yes I have real appreciate your courageous it is good for
competent presenters
MAENDELEO YAKO BINAFSI YATALETWA NA WEWE BINAFSI.
Na, Audax Ikwataki
0765090379
Na ili uweze kufikia maendeleo unatakiwa kutokumlaumu mtu yeyote kwa jambo lolote hata kama amehusika moja kwa moja katika kusababisha wewe kutokufikia malengo flani badala yake jilaumu mwenyewe kwa kushindwa kupanga mikakati madhubuti ya namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Utawezaje kufikia maendeleo?
Unatakiwa kujisimamia(Self Management) na kujiongoza (Self Leadership) mwenyewe katika kufanya maamuzi sahihi lakini kwa kuzingatia weledi, uadilifu, uaminifu na matumizi sahihi ya maarifa(knowledge), ujuzi (skills) na mawazo (ideas) uliyonayo ili kuleta ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili jamii bila kuvunja sheria zilizowekwa.
Kumbuka, kila mtu ana maarifa, ujuzi au wazo flani hivyo huwezi kujitoa katika nafasi ya kujiletea maendeleo wewe binafsi.
Ebu kwanza jiulize, ni mara ngapi nafasi za juu zimetangazwa ndani ya kampuni unayofanya kazi na zimekupita kwasababu huna vigezo? Umewahi kuwaza kujisimamia na kujiongoza katika kuboresha ufanisi wako katika kazi au kuongeza kiwango cha elimu au ujuzi wako ili kukidhi vigezo vya nafasi za juu?
Kwa wale ambao mmemaliza elimu ya chuo kikuu na hamna kazi, je, umewahi kujiuliza ni mara ngapi jamii imekuwa ikihangaika kutafuta suluhisho la jambo flani ambalo kwa elimu yako uliyoipata una majibu ya tatizo hilo lakini umekaa tu unasubiri uajiriwe ofisini?
Kwa wewe ambaye una wazo flani ambalo ni jibu la hitaji la jamii, umewahi kujiuliza ni mara ngapi jamii imekuwa ikitafuta mtu wa kutoa huduma(services), bidha(products) au suluhisho(solution) ambayo wewe unawaza tu na kukaa kimya?
Unatakiwa kijiuliza na kuchukua hatua ya kufanya maamuzi kwa kuzingatia yaliyotajwa hapo juu.
Na,
Audax M. Ikwataki
audaxmuga@yahoo.com
Post a Comment