Wednesday, 4 April 2018

VITABU VITANO VYA KUSOMA KWA KILA MJASIRIAMALI NA MFANYABIASHARA



Kama wewe ni mjasiriamali na mfanyabiashara ambaye hasomi vitabu naweza kusema ni mfanyabiashara aliyepitwa na wakati. Katika karne ya ishirini na moja mambo yamebadilika  kila kukicha kuna mambo mapya yanajitokeza ambayo kama huyajui yataathiri mwenendo mzima wa biashara yako.



Hivyo huna budi kuwa mtu wa kusoma vitabu na kutafuta maarifa yaliyo vitabuni humo. Kama tajiri namba moja duniani Bill Gates anafahamika kwa kuwa msomaji mzuri wa vitabu unafikiri huwa anataka kujua nini kama si kutafuta maarifa yatakayo msaidia kuendeleza biashara zake. 

Warren Buffet mwekezaji namba moja duniani hutumia zaidi ya nusu ya muda wake kusoma vitabu. Wewe pia unahitaji kujenga tabia mpya ya kusoma vitabu kama una ndoto ya kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa. Binafsi nimejifunza mengi kwenye biashara zangu baada ya kuwa msomaji wa vitabu.
 
Leo hii nataka nikupe orodha ya vitabu vinavyozungumzia biashara na ujasiriamali vilivyoandikwa na waandishi mahiri wa Kitanzania ambavyo nakushauri uvisome.

Ifuatayo ni orodha ya vitabu ambavyo kila mjasiriamali na mfanyabiashara anatakiwa kuvisoma: 

  • BIASHARA NDANI YA AJIRA - Makirita Amani
Kuwa na chanzo kimoja cha kipato ni jambo la hatari sana. Kutegemea chanzo kimoja kujipatia kipato ni jambo la kutisha sana na si rahisi kuufikia uhuru wa kifedha. Hivyo mwandishi anaeleza kuwa unaweza ukawa ndani ya ajira lakini bado unafanya biashara inayokuingizia kipato kizuri  tu. Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba ukitaka kuanza biashara Fulani kama una kazi basi lazima uiache. Makirita Amani ameeleza vizuri namna unavyoweza kuimili mzani wa kazi na biashara. Usiache kusoma kitabu hiki hasa kama umeajiriwa na una ndoto ya kufanya biashara.

  • 2.   BIASHARA & UJASIRIAMALI - Lazaro Samwel
Lazaro Samwel ni mwalimu mzuri wa masomo ya ujasiriamali. Katika kitabu chake cha biashara na ujasiriamali nimepata kumjua mjasiriamali ni mtu wa namna gani. Namna ya kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio. Jinsi ya kupata mtaji wa biashara. Jinsi ya kupata wazo la biashara na jinsi ya kupata na kupanua soko. Katika kitabu hiki mwandishi ameeleza jinsi alivyoweza kuuza nakala 200 za kitabu chake cha NGUZO 3 ZA MAISHA kwa w

atu aliofahamiana nao kwenye mitandao ya kijamii, mimi nikiwa mmoja wao. Unataka kujua aliwezaje? Jipatie kitabu hicho kwa kuwasiliana na mwandishi LAZARO SAMWEL kupitia 0653386586.
 

  • 3.   MISINGI YA UJASIRIAMALI ILIYOFANIKISHA WATU WENGI DUNIANI – Adabert Chenche
Katika kitabu hiki utajifunza misingi mbalimbali ambayo ukifata itaweza kukufanya mjasiriamali mwenye mafanikio. Adabert anaamini yakwamba wazo lako moja linaweza kukupeleka kwenye mafanikio. Kupata kitabu hiki wasiliana na Adabert Chenche kupitia 0712957528.
 

  • 4.   MPENYO (Jinsi Ya Kufanikiwa Kifedha Katika Hali Ngumu Ya Uchumi) – James Mwang’amba
Leo hii kila unayekutana naye anakwambia “VYUMA VIMEKAZA.” Kocha Mwang’amba amekuletea shuluhisho ya kusema vyuma vimekaza na njia pekee ni kusoma kitabu chake cha MPENYO na kuchukua hatua kwa yale aliyoyaandika. Sio kila hatua huleta furaha lakini bila kuchukua hatua huwezi kupata furaha.
 

NAMNA YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO UNASOMA - EDIUS KATAMUGORA
 
Hiki ni kitabu kinachomuandaa mtu yeyote anayetamani kuwa mtaalamu katika sekta fulani. watu wanafanya biashara na wabobezi. Ukiwa mbobezi katika sekta fulani watu watakuwa tayari kukulipa na utatengeneza pesa nyingi. Jifunze sasa unavyoweza kuwa mtaalamu kwa kuanza kusoma kitabu hiki. Piga simu: 0764145476 utaletewa mahali ulipo.

Mafanikio Yako Mikononi Mwako.

Ndimi:
Edius Katamugora

0764145476
ekatamugora@gmail.com     

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: