Wednesday, 8 March 2017

Makosa Yako Ya leo Ni Makosa Yako Ya Kesho.


Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na upo tayari kupambana kutimiza ndoto zako katika siku ya Leo.

Karibu sana katika mada ya Leo "Makosa yako ya Leo ni makosa yako ya kesho".

Mara nyingi tunapofanya kosa Fulani tunajitahi kulikwepa na kutolisahihisha au tunajifanya kana kwamba halijatokea kabisa. Hii si tabia nzuri maana itatuponza mbele ya safari.

Kuna sehemu unafanya kitu unagundua umekosea lakini unaacha tu uwezi kufanya jitihada zozote kusahihisha. Tulipokuwa wadogo tunajifunza kutembea mara nyingi tulianguka lakini wazazi wetu walituacha tu bila kutuhurumia na hatimaye tulijua kutembea. Au kumbuka kipindi unajifunza baiskeli ulianguka mara ngapi lakini hukuacha, Leo hii unaendesha baiskeli vizuri.

Unapofanya kosa Fulani kumbe huna budi kulirekebisha kabla hata halijawa kubwa. Tuchukulie kwa mfano mwanafunzi wa kidato cha kwanza hasiyependa somo la hesabu, huyu akiendelea hivi kidato cha NNE moja kwa moja atapata alama "F", kumbe tunapoacha kushughulikia makosa yetu yakiwa mabichi tunayaacha yakomaa na hatimaye tunavuna matunda yanayotutumbukiza shimoni. Waswahili wanasema "Usipoziba ufa utajenga ukuta". Na kufanya kosa sio kosa Bali kurudia kosa.

Uchunguzi uliofanyika unasema kila sekunde 0.25 kosa linapofanyika kuna mambo mawili: mtu anaweza kulitupilia mbali bila kulishahihisha au anaweza kulisahihisha. Yule anayesahihisha kwa kiasi kikubwa ubongo wake unaongeza ufanisi katika kutenda. Bwana Thomas Edson ambaye ndiye aligundua taa inayowaka kwa Umeme alifanya majaribio zaidi ya elfu kumi bila kufanikiwa lakini hakukata tamaa. Leo hii ndiye Baba wa Umeme duniani.

Makosa yanakufanya ukue kimtizamo na kiakili kama utakuwa tayari kuyarekebisha. Hata kama ukifanya bila kufanikiwa kuna sehemu fulani utakuwa umepiga hatua ingawa huioni. Ni bora kuwa na mwendo wa kobe kuliko kubaki pale pale ulipo. Ukiacha makosa unayofanya leo na kuyadharau bila kuyafanyia kazi ni kama unaacha kidonda bila kukitibu na baadaye kinakuwa jibu. Kipi bora kati ya kidonda au jipu?. Tafakari chukua hatua.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia Makala moja kwa moja).
Email; ekatamugora@gmail.com
Facebook page; bideismblog (like page yetu)

"See you at the top".

Karibu tena kusoma Makala nzuri kama hizi katika blog hii.

Tangazo;
Nimeandika Kitabu kinachoitwa "Barabara Ya Mafanikio" unaweza kuweka oda yako mapema kwani nakala ni chache.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: