Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea vizuri na majukumu yako. Nikukumbushe kwamba leo ni siku yako muhimu sana kwako usikubali ipotee. One day can make you grow.
''Amini, nawaambia mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka ukatupwe baharini, litatendeka." (Mathayo 21:21).
Amini na amini kwamba unaweza kuamisha mlima na unaweza kwa asilimia mia. Watu wengi hawaamini kwamba wanaweza kuhamisha milima na wanajikuta hawafanyi hivyo.
Katika dunia hii ya leo kuna watu wengi waliohamisha milima na kuitupa baharini. Hawa ni watu wenye imani. Na katika sheria za asili zilizokuwepo toka miaka elfu kabla ya Kristu ni sheria ya uvutano ( law of attraction) kwenye sheria hii iliyojigawa Mara tatu, imani imesimama kama nguzo ya tatu.
Kuamini kuna nguvu kubwa katika maisha ya mwanadamu na sio nguvu tu ata miujiza.
Imani inafanya kazi namna hii;
Ukiwa na imani kwamba "nipo chanya na naweza" mtizamo, unatoa msukumo wa nguvu na ujuzi unaofanya jambo Fulani, ukiwa na imani kwamba " naweza kufanya jambo Fulani" namna ya kufanya jambo hilo inajileta yenyewe.

Zamani watu waliamini barua ni nusu ya kuonana. Lakini Alexander Graham Bell alikuwa na imani zaidi akaisaidia dunia kugundua simu. Hatutumii tena barua kwa kiasi kikubwa.
Watu hawakuamini kwamba mtu anaweza kuelea angani. Wright Brothers kuziilisha jambo hilo wakaamua kutengeneza ndege. Leo hii tunaelea angani.
Isingekuwa imani nadhani hadi leo hii tungekuwa tunatumia vibatari na chemli. Bwana Edson Thomas ilimpasa afanye majaribio zaidi ya elfu moja ndipo alipogundua taa inayotumia umeme, maarufu kama balbu ( light bulb). Ni imani iliyoje!.
Henry Ford alikua na imani na picha ya gari lenye kutumia silinda nane. Mainjia wake walimwambia zaidi ya Mara 5 kwamba haiwezekani. Yeye aliwaambia linawezekana. Hatimaye aliwalazimisha hadi wakapata uwezo wa kutengeneza gari hilo. Leo tunaona V8 zinanesa tu barabarani. Lakini mwanzoni hata mainjinia walijua gari hilo haliwezi kutengenezwa. Ni kutokana na imani ya Ford tu jambo hili limewezekana.
Chrispher Columbus aliamini kwamba kuna kuna dunia mpya ( new world) ..Ndiyo dunia tunayoishi leo hii.
Chrispher Columbus aliamini kwamba kuna kuna dunia mpya ( new world) ..Ndiyo dunia tunayoishi leo hii.
Mwaka 1952, Bwana Edmund Hillary alishindwa kupanda mlima Everest wenye futi 29,000 kutoka usawa wa bahari, baada ya kushindwa alichukua picha ya mlima huu na kusema maneno haya "Mlima Everest, ulinipiga siku ya kwanza, lakini nitakupiga siku zinazofuata, kwakuwa umekua kufikia ukomo, lakini Mimi naendelea kukua."
Kwa imani hii hatimaye tarehe 29, mei mwaka 1953 aliweza kuwa mtu wa kwanza duniani kupanda mlima Everest. Kuna nguvu kubwa katika imani na kile unachokiamini. Ukisoma pia historia ya Abraham Lincoln utagundua alikuwa na imani kubwa. Ni mtu aliyekosa nafasi nyingi za uongozi lakini akuchoka kugombea na hatimaye alipata kuwa raisi wa Marekani.

Watu wengi waliofanikiwa wanaongozwa na imani, kila siku wanang'oa milima na kuitupa baharini. Hata wanasayansi pia wanaongozwa na imani katika kufanya majaribio yao ndio maana wanaendelea hawaachi kwani wanaamini kuna kitu watakigundua.
" Amini nawaambia mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya sio hilo la mtini tu, lakini hata mkiuambia mlima huu, Ng'oka ukajitupe baharini, litatendeka." Mathayo 21:21
Ask-belive-receive (Law of attraction).
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Usisahau kuunganisha email yako hapo chini ya Makala hii.
"See you at the top."
0 comments:
Post a Comment