Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa makala za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na u mzima wa afya. Nakukumbusha kwamba Leo ni siku muhimu usikubali ipotee hivi hivi. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala ya Leo niliyokuandalia. Jana nilipata Bahati ya kuuzulia semina chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya. Semina hii iliendeshwa na King Chivala ambaye ni muhamasishaji na kocha wa ujasirialiamali na mafanikio. Katika zungunguza yake kwenye semina hii King Chivala alisema maneno ambayo nimeyafanya kichwa cha Makala hii, yaani "wewe ni bustani, unachokitafuta ni kipepeo." Kwenye maisha tunatafuta vitu vingi, wengine Mali, marafiki, ufaulu, wachumba n.k. lakini tunasahau kwamba sisi ni bustani na tunachokitafuta ni kipepeo. We we ni bustani pesa ni kipepeo, wewe ni bustani mchumba unayemtafuta ni kipepeo.
Wengi wetu nadhani tunatambua na kuwajua vipepeo, wao upenda bustani nzuri na zenye maua mazuri na hivyo kuweza kuwavutia vipepeo. Hivyo ndivyo maisha yetu yanavyopaswa kujengwa kwa misingi hiyo. Kila kitu kizuri kiandalie mazingira na utakivutia kwako. Unataka uwe na pesa lakini matumizi yako yanazidi kipato chako!, au unataka marafiki wazuri wakati wewe mwenyewe umejaa tabia mbovu!, unategemea nani awe rafiki yako. Au unatafuta mchumba mzuri Mwenye tabia njema na mtaratibu, wakati wewe ujatulia hata kidogo, watakukimbia tu na utaishia kusema nina mkosi. Kumbe unachokitafuta kinakutafuta. Kilichobaki ni wewe kukiwekea maandalizi na kukipokea kwa mikono miwili na zulia jekundu. Jitahidi kuwa bustani na utapata vipepeo wengi wa kila aina.
Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Usisite kulike page yetu ya Facebook na kujiunga na mfumo wetu wa e-mail hapa chini.
"See you at the top."
0 comments:
Post a Comment