Friday, 14 April 2017

Usiishi Maisha Ya Chura

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kwenda kutimiza ndoto zako Leo. Nikukumbushe pia kwamba Leo hii ni siku muhimu kwako usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu katika Makala ya Leo inayosema "usiishi maisha ya chura." Kuna hadithi ya mwalimu mmoja aliyemchukua chura na kumuweka kwenye chungu na baadae alikiweka kile chungu jiko lililokuwalikiwaka moto. Mwalimu alifanya kitendo hiki Mbele ya wanafunzi wake. Baada ya maji kuanza kupata joto kidogo chura huyo alikuwa akifurukuta furukuta ndani ya maji. Maji yalipata joto sana na hatimaye chura aliishiwa nguvu za kufurukuta na huo ndio ukawa mwisho wake.

Kisha baada ya wanafunzi kutizama tukio hilo mwalimu aliwauliza wanafunzi wake swali ili. Ni nini kilimuua chura?. Wote wakajibu "Ni maji ya moto." Mwalimu akawaambia wote yakwamba wamekosa. Jibu ni kwamba kilichomuua chura ni uzembe wake. Kabla maji hayajachenka sana chura huyo alikuwa na nguvu za kuruka na kutoka kwenye  chungu lakini alitumia nguvu hizo kutumia mwili wake ulingane na lile joto la maji. Mwisho wa siku joto la maji lilizidi joto la mwili wake na hatimaye kufa, huku akiwa hana uwezo wa kuruka tena kwani mwanzo alitumia nguvu kidogo kulinganisha joto la mwili wake na lile la maji, maji yalipozidi hakuwa na nguvu tena.

Tujifunze nini?
Kutoka na hadithi hii tujifunze kabisa kuacha kuishi maisha aliyoishi chura. Mwanzoni kabla maji hayajachemka ni sawa na kulinganisha na ujana wetu. Kipindi cha ujana ndicho kipindi ambacho tunakuwa na nguvu nyingi za kujishughulisha, uwezo mkubwa wa kifikiri lakini hatuutumii. Kwenye ujani ndipo inabidi tupambane kuitengeneza kesho yetu, ndipo inabidi tuwekeze katika nyanja mbalimbali lakini hatufanyi hivyo.

Umri ukipita na kuzeeka tunakosa nguvu hatuwezi kufanya mambo makubwa kama umri wa ujana wetu. Tunafanana na chura akiyezidiwa ubabe na maji ya moto tunakufa huku tukijiona. Hivyo basi kumbe umri wa kuwa kijana ni umri wa kufanya mambo makubwa na ya ajabu tusikubali upotee hivi hivi. Watu walio utumia ujana wao vizuri Leo hii ndio dunia inawashangaa, Bill Gates alikuwa na miaka 16 alipogundua software ya komputya akiwa na mwenzake Allen aliyekuwa na miaka 19. Leo hii nani asiyeijua kampuni ya Microsoft?.

Kumbe umri wa ujana ni umri wa kupambana kutengeneza kesho zetu. Waingereza wanamsemo unaosema "Life begins at forty" wakimaanisha "maisha yanaanza ukiwa na miaka 40." Hapa wanamaanisha nini?, ukiwa na miaka arobaini hakikisha unavyanzo vyako vya mapato kama kazi,biashara n.k, umeacha kusoma na unasomesha, umejenga Nyumba na unaishi kwako. Umewekeza katika maeneo mbalimbali kama ardhi,his a n.k. Kama unafanya kazi kwenye serikali au kampuni Fulani una uwezo wa kustaafu na kuanza  kufanya shughuli zako binafsi.Hii ndiyo maana halisi ya "life begins at forty." Kwa Tanzania kijana ni Mwenye umri kuanzia miaka 18-35. Kumbe ni katika umri huu inatubidi tuhakikishe tunafanya mambo makubwa kwani tunakuwa na nguvu nyingi na hivyo tusikubali kuishi maisha ya chura..

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Email; ekatamugora@gmail.com
0764145476
0625951842 (whatsapp)
Kumbuka kujiunga na mfupo wetu wa email hapa chini na pia kulike page yetu ya Facebook.

"See you at the top."

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: