Habari za asubuhi mpendwa
msomaji wa BIDEISM BLOG.
Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kwenda kutimiza
majukumu yako ya leo na kuongeza kitu Fulani kitakacho kusaidia kutimiza ndoto
zako. Leo ni siku muhimu sana usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala
nzuri ya leo niliyokuandalia.
Leo hii ningependa
kuongelea kitu muhimu katika biashara na ujasiriamali. Kitu hicho ni HUDUMA. Wafanyabiashara wengi na
wajasiriamali wengi hasa wale wanaoanza biashara, biashara zao huanguka na
kurudi nyuma kwa sababu hawalizingatii jambo hili. Wengi wanatanguliza pesa
kwanza na kusahau kutoa huduma bora.
Leo nataka nikwambie
kwamba hakuna kitu muhimu kwenye biashara kama huduma unayoitoa kwa wateja
wako. Ukiwa kama mjasiriamali au mfanya biashara tanguliza kwanza huduma na
pesa zifuate. Toa huduma bora, uziwe mtu wa kuwaza pesa kabla ya kuwapa wateja
wako huduma nzuri.
Watu wengi wamekuwa
wakiyaamini makampuni makubwa na kuwa wateja wa kampuni hizo kwa sababu ya
huduma nzuri wanazozipata kutoka kwenye kampuni hizo. Ingawa wakati mwingine
kampuni hizo zinawatoza pesa nyingi lakini wajikuta wanalipia kiasi kizuri kwa
sababu ya huduma nzuri wanazozipata.
Umewahi kufikiria kwanini
kuna hoteli baadhi wanauza glasi ya juisi ya embe kwa shilingi elfu tano na
sehemu nyingine glasi kama hiyo hiyo ya
embe wanauza shilingi mia tano na watu wapo tayari kwenda kununua sehemu
wanakouza elfu tano na kuacha sehemu inapouzwa juisi kama hiyo kwa shilingi mia
tano.
Faida ya kutoa huduma
nzuri ni kwamba watu watakuja kwako tu ingawa muda mwingine unakuwa na bei za
juu kuliko wenzako. Kuna mtu aliwahi kusema “Give good service to all people and when they come, bill them.” Akimaanisha, “Toa huduma nzuri kwa watu na wakija kwako
kununua watoze pesa.”
Faida nyingine ya kutoa
huduma nzuri ni kwamba utaongeza wateja. Hii ipo hivi, akija leo mtu Fulani
kwenye biashara yako ukampa huduma nzuri, atakwenda kuwaambia wenzake huduma
nzuri unayoitoa, na wateja wataanza kuja kwako kuangalia kama kweli unatoa
huduma nzuri waliyoambiwa. Wakija na kukuta jambo waliloambiwa linatendeka,
watakuwa wateja wako pia, hivyo hivyo watawaambia na wengine.
Wafanya biashara wengine
wamekuwa na tabia za kutapeli, wamesahau kwamba dunia ni duara. Utamtapeli mtu
hapa leo na utakwenda kukutana nae sehemu nyingine. Usiwahi kufanya biashara ya
dhuruma hata siku moja, hapo pia unajiwekea mikosi katika biashara zako.
Wajasiriamali na wafanya
biashara wengine wamekuwa wakijisahau kidogo, yaani wanaanza na huduma nzuri na
baada ya kupata pesa wanasahau kile wanachokifanya na kuacha kutoa huduma
nzuri. Kumbuka watu walikuja kwenye biashara yako kufuata huduma nzuri na si
vinginevyo. Kama ni mama nitilie, watu walikuja kwako kwa sababu tu ulikuwa
ukipika chakula kitamu na kizuri. Wataondoka kwako endapo utabadili ladha na
kuanza kupika ovyovyo. Kama ni fundi viatu, watu walikuja kwako kwa sababu tu
ulikuwa ukiwashonea viatu vyao vizuri, lakini leo umekuwa ukifanya ilimradi tu
liende, wateja wako watakukimbia. Hii inatumika kila mahali kwenye biashara
yeyote.
Kwenye kitabu kinachoitwa
“Marketing Insights From A To Z”, mwandishi Philip Kotler, ameanza na maneno
haya kwenye utangulizi, “Tatizo kubwa
leo hii katika bishara, sio kukosekana kwa bidhaa bali ni kukosekana kwa wateja.”
Na wateja wanakosa kwasababu ya huduma mbovu zinazotolewa na wafanya biashara
na wajasiriamali katika shughuli zao.
Daima kumbuka kutoa
huduma nzuri kwanza halafu baadaye ndipo pesa ifuate, usibadili fomula hii
kwenye biashara yako, toka unapoanza na kila siku kumbuka jambo hili.
Ni mimi rafiki na ndugu
yako
EDIUS BIDE KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL
SPEAKER
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com
KARIBU SANA KUWEKA ODA YA
KITABU CHANGU KIZURI KINACHOITWA “BARABARA YA MAFANIKO”. NI KITABU KIZURI
KINACHOONGELEA MENGI KUHUSU MAFANIKIO.
Washirikishe na wenzako
kile ulichojifunza, kwani ni muhimu kwao pia.
0 comments:
Post a Comment