Wednesday, 24 May 2017

Kila Aliyefanikiwa Amesaidiwa Na Aliyefanikiwa

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala nzuri ya Leo niliyokuandalia.

Umewahi kusikia mtu akisema "asingekuwa mtu Fulani mimi nisingekuwa hapa." Katika safari ya mafanikio kuna watu wanaokutoa sehemu moja na kukusaidia kukupeleka mahali pengine.
Jifunze kujikutanisha na watu waliofanikiwa katika nyanja Fulani ambayo wewe ni Mgeni na unatamani kufanikiwa katika nyanja hiyo. Ukijifunza kwa watu waliofanikiwa watakupa mwongozo bora na ramani itakayokusaidia kufika kule unakotaka.
Watu waliofanikiwa watakufundisha namna ya kukumbana na matatizo mbalimbali kwani ukiona nyani kazeeka, tambua amekwepa mishale mingi.

Watu waliofanikiwa watakusaidia kutengeneza daraja ata kama mto ni mkubwa kiasi gani na utaweza kuvuka. Jifunze kujikutanisha na watu waliofanikiwa na pia kuwa tayari kujifunza kutoka kwao. Kuwa na urafiki na watu waliofanikiwa.

Kwenye Kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio nimeandika, "watu unaotumia nao muda mwingi unakuwa kama wao." "You become like people you hang out with." Kumbe ukikaa na watu waliofanikiwa utajifunza mengi kuhusu mafanikio.

Ukweli ni kwamba watu waliofanikiwa wako tayari kukufundisha kama utakuwa tayari kujifunza. Kama utakuwa makini na mtu mwenye utayari. Vinginevyo hawatakuwa tayari kukufanya wewe mmoja wao. Kwani "ndege wenye mbawa sawa huruka pamoja." Ni msemo wa kiingereza.
Kuna aliyewahi kusema "fuata mto unaweza kukutana na bahari." Kumbe hivyo hivyo fuata watu waliofanikiwa wakufundishe mafanikio, wakufundishe kufanikiwa.

Nakumbuka baada ya kujuana na kaka Lazaro Samweli ambaye ni mwandishi wa Kitabu kinachoitwa Nguzo Tatu Za Maisha nilimuomba anifundishe namna ya kuandika kitabu, naye hakusita kunifundisha. Leo hii namshukuru Mungu nimeweza kuandika Kitabu changu kinachoitwa Barabara Ya Mafanikio.

Mwanafilosofia Plato anajulikana kwa kuwa mwanafilosofia mzuri lakini alifundishwa na mwanafilosofia Socrates. Plato akuishia hapo tu alimfundishwa mwanafalsafa mashuhuri Aristotle.

Pattie Mallete ni mama yake Justine Bieber ambaye ni mwimbaji maarufu wa muziki kutoka nchini Canada. Akiwa bado kijana Alipenda sana kuimba na kuigiza lakini hakuweza kufanya vizuri.tarehe 1 machi 1994 alimzaa mtoto wake wa kwanza Justine BIEBER. Mwanae baada ya kuonesha kupenda kuimba toka akiwa na miaka miwili alijitahidi kumfundisha kuimba na alimtafutia vifaa vya kucheza muziki kama gitaa. Justine akuweza kutumia mkono wa kulia kucheza gitaa hivyo ilimpasa mama yake amtafutie gitaa la kushoto. Mwaka 2007 alimuingiza mwanae katika mashindano ya kuimba yaliyojulikana kama ''STARTFORD STAR'' ambapo aliibuka mshindi wa pili baada ya kuimba wimbo wa msanii Ne-Yo wa Marekani. Leo hii Justine ni mwanamuziki maarufu duniani.Mwaka jana alitamba na kibao chake kilichojulikana kwa jina la ''SORRY''. Kila aliyefanikiwa amefundishwa na aliyefanikiwa.

See you at the top
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author, inspirational and motivational speaker.
0764145476
0625951842 (whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Karibu sana kuweka oda ya Kitabu kizuri chenye mafundisho mengi mazuri kuhusu mafanikio kinachoitwa Barabara Ya Mafanikio.

Usisahau kuwashirikisha wenzako yale uliyojifunza ili yapate kuwafikia wengi.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Unknown said...

Sawa nzuri hiyoo!!!!