Wednesday, 10 May 2017

                                                             

Habari mpendwa msomaji wa makala za Bideism Blog. Ni mtumaini Yangu kwamba umeamka salama na u mzima wa afya. Ni siku nyingine tena ambayo tumepewa ili kufanya kwa bidii na juhudi ili kutimiza ndoto zetu. Leo ni siku muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu katika Makala ya leo niliyokuandalia.
Leo napenda kuongelea malezi ya watoto na miaka ambayo watoto wanaweza kujifunza.
Katika ukuaji wa mwanadamu kuna makundi matatu ambayo kila mwanadamu anaweza kupitia katika kujifunza. Makundi hayo yamegawanyika kwenye miaka, kadri ya mtu anavyokua.
Makundi hayo ni kama yafuatayo.
(1) umri wa kuzaliwa mpaka miaka 12
(2) miaka 12-24
(3) miaka 24-36

Umri wa kuzaliwa hadi miaka 12, #1

Katika kipindi hiki cha ukuaji mtoto huwa kama mashine ya kujifunza. Wazazi hawatumii nguvu nyingi kumuhasa mtoto kujifunza. Watoto wenyewe upenda kujua vitu kama kutambaa, kutembea, kujifunza kula na kuendesha baiskeli.
Ni katika kipindi hiki mtoto hujifunza lugha mbalimbali. Muda huu ni muda mzuri wa kumfundisha mtoto mambo mengi na atakuwa tayari kujifunza.


Kundi la pili #2

Miaka 12-24 ( kujifunza kwa kulazimishwa/ kugomesha)
Katika kipindi hiki mtoto uingia kwenye umri wa kubalehe, na hapa wanajifunza kwa kugomesha Mara nyingi. Ukimwambia Fanya hivi yeye anafanya kinyume chake.
Mfano ukimwambia anapoendesha gari hasilikimbize yeye anapopata Uhuru anakimbiza.
Katika kipindi hiki watoto wengi hupenda kujifunza wanachopenda kujifunza zaidi ya kile walichoambiwa. Wanaanza kutumia nguvu zao za kufikiri na kufanya chaguzi wao wenyewe bila wazazi.
Ni katika kipindi hiki ambacho vijana na watoto wengi wanajiingiza katika makundi yasiyofaa, kama wakabaji, makahaba, uteja, uvutaji bangi kutaja machache.
Kama mtoto akipita kwenye umri huu na kuonesha mambo chanya, mara nyingi yupo katika wakati mzuri wa kufanya vizuri maishani
.
Kundi la tatu #3
Miaka 24-36 ( kujifunza kwa ajili ya kazi)
Huu ndio muda ambapo mtu mzima anatengeneza maisha yake. Hiki ni kipindi muhimu sana katika kujifunza.
Katika kipindi hiki mtu, anaanza kuota mizizi iliyokomaa kwenye kujifunza kuhusu kazi yake atakayoifanya. Kwa mfano kama alikwenda kwenye chuo cha uuguzi, atagundua kama yeye ni daktari mzuri au la. Wanagundua kama walichagua kazi sahii.
Kama mtu akwenda chuo au kujifunza kitu chochote cha kumpatia kazi, watu wengi hapa uanza kufanya kazi mbalimbali. Leo utamkuta hapa kesho kule. Watu wengi hapa upata ujasiri wa kufuata mdoto zao. Muda huu ndio vipaji vingi vya watu uanza kuonekana.
Kipindi cha kwanza ni muhimu sana kwenye malezi ya watoto kwani ndiyo msingi wa maisha yao. Samaki mkunje angali mbichi. mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hivyo wazazi wanapaswa kutilia sana mkazo mtoto akiwa amezaliwa hadi kufikia miaka 12.
Ni mimi rafiki na ndugu yako.

Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini na pia kujiunga na mfumo wa email hapa chini ili upate Makala hizi moja kwa moja.

Washirikishe na wenzako.

See you at the top

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: