Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiandaa kwenda kuyatimiza majukumu yako siku ya Leo. Leo ni siku muhimu, usikubali kuipoteza bure. One day can make you grow.
Karibu sana katika makala ya Leo niliyokuandali. Watu wengi wamekuwa wakitenda mambo mema kwa wale watu wanaowafahamu au wenye vyeo Fulani. Huu ni mtizamo hasi ambao inabidi jamii zetu ziachane nao.
Mara nyingi unaweza kukuta mtu anampa msaada mtu Fulani kwa sababu anafahamiana naye. Hii inaleta mtizamo hasi kwa watu wengine. Unapojifanya kuwa mwema kwa bosi wako na kuwafanyia wengine ndivyo sivyo kumbuka hata bosi wako alianzia huko chini.
Kumbe siku moja mtu uliyekuwa ukimfanyia mabaya ndiye atakuja kuwa bosi wako.
Wazazi wengine wamekuwa wakiwanyima watoto wao mambo Fulani Fulani na kuwaendeleza wengine. Mfano unakuta mtoto Fulani ananyimwa kitu Fulani na wengine wanapata. Kuna watu wengine huko nyuma wazazi wao walikataa kuwasomesha lakini Leo hii ndio kitega uchumi cha familia. Wale waliosoma hawazisaidii familia zao. Kumbe wazazi wanayo haja ya kutoa malezi yaliyo sawa kwa kila mtoto.
Kila mtu unayekutana naye kila siku mtendee wema, hujui siku moja atakuwa nani.
au utamkuta wapi. Kwenye biashara jambo ili ni muhimu sana jali sana Wateja wako wote hata kama ni wa siku moja. Kumbuka watu wananunua kwa mtu wanayemjua na kumuamini. Sasa kama huwatendei watu mambo mema unategemea kweli waje kwenye biashara yako kama Wateja?.
Kumbe inatubidi tubadilike. Tujali kila mtu na tusibaguane. Tenda wema nenda zako.
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author & Motivational Speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com
Edius Bide Katamugora
Author & Motivational Speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com
See you at the top
Usisahau kulike page yetu ya Facebook @bideismblog hapa chini.
0 comments:
Post a Comment