Habari mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba u mzima na mwenye afya tele. leo ni siku muhimu sana usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika makala ya leo niliyokuandalia.
leo ningependa kuongelea mavazi. Katika karne hii ya ishirini na moja watu wengi wanaangalia sana unavaaje ndiyo maana nikakipa kichwa cha makala hii, watu wanahukumu kava ya kitabu.
Watu wengi wanategemea kitu unachokifanya kinaendana na mavazi unayovaa au jinsi unavyovalia ndivyo inavyopaswa kuwa katika jamii.
Kuna wengine wameendekeza misemo ya kijinga na kusema "utajiju'' au simvalii mtu yeyote lakini sio misemo ya kuendekeza kabisa.
Kuna wakati niliwahi kuandika kuhusu kuweka alama na katika kipengela cha uvaaji kinahusika kwa maana kubwa. Watu wakisema yule ni mwalimu, tunategemea uvaaji wako sio wa kumkwaza mwanafunzi.
Au wakisema yule ni mhamasishaji tunategemea muonekano wako utarandana na ule wa wahamasishaji wengine, na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu. jali sana mavazi yako kwani yanaweza kukupunguzia adhi fulani mbele za watu, hasa watu wapya unaokutanishwa nao.
Kuvaa vizuri ni njia pia ya kuweka alama njema(branding yourself).
Mhamasishaji mashuhuri kutoka Marekani, Les Brown aliwahi kusema "Wear like a prospect, not like a suspect." akimaanisha, "Vaa kama mtarajiwa, usivae kama mtuhumiwa." Hii itakusaidia sana, mfano ikitokea sehemu wameiba labda simu, ya mtu, na wewe umevalia vibaya vibaya, mtu wa kwanza kumtaja kama mwizi atakuwa aliyevalia vibaya.
Kuna mtu aliwahi kusema "It pays to be smart." akimaanisha "inalipa kuwa mtanashati,"
See you at the top
Ni mimi rafiki na ndugu yako.
EDIUS BIDE KATAMUGORA
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email:ekatamugora@gmail.com
Karibu kuweka oda ya kitabu cha BARABARA YA MAFANIKIO
0 comments:
Post a Comment