Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Tumshukuru Mungu kwa siku nzuri kama ya Leo. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza ndoto zako siku ya leo. Leo ni siku muhimu husikubali ipotee.
Karibu sana katika makala nzuri ya Leo niliyokuandalia.
Leo hii tunaendelea na makala ya jana Kama nilivyokuahidi. Kama ukusoma makala ya jana bofya hapa kuisoma: http://bideism.blogspot.com/2017/06/huitaji-umri-mkubwa-kufanya-makubwa.html
Jana nimeweza kueleza mfano wa mtoto mikaila. Najua kuna kitu kikubwa umeweza kujifunza kutoka kwake.
Leo ningependa pia kukupa picha ya mtoto mwingine ambaye anafanya makubwa katika karne hii ya ishirini na moja. Anaitwa Nyeeam Hudson ni raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 12. Anajulikana kwa jina maarufu kama King Nahh. Mtoto huyu ni mhamasishaji na amekuwa akizunguka dunia nzima kuwahamasisha watoto wenzake na wazazi pia. Mwaka jana 2016 alifika Tanzania. Hekima na uwezo alionao unaweza kusema labda ana miaka 40. Amekuwa akisoma vitabu ambavyo vimemsaidia sana kufika hapo alipo. Ukiingia instagram au You tube na kumuangalia King Nahh nafikiri utaweza kupata picha halisi ya ninachokisema hapa.
Pamoja na umri huu mdogo ameweza kuandika kitabu kinachoitwa "We are all Kings" ni bidii iliyoje.
Nchini Uganda pia kuna kikundi kidogo cha watoto yatima ambao wamekuwa wakicheza muziki kwenye matamasha mbalimbali na pia video mbalimbali. Watoto hawa wanajulikana kama Ghetto Kids. Wameweza kutengeneza pesa nyingi na wametembea katika nchi nyingi kufanya shoo nyingi tu za kimuziki. Kweli huitaji umri mkubwa kufanya mambo makubwa.
Kumbe hakuna umri Fulani ambao umetengwa wa sisi kuanza kufanya makubwa. Kama ni kipaji chako anza kukionesha mapema. Waingereza wanasema "practice makes perfect" wakimaanisha, mazoezi huleta utimilifu. Anza sasa kufanya mambo makubwa. Amka kwenye wimbi la watu wengi wanaosema nitaanza kufanya jambo Fulani nikifikia umri Fulani. Kusitasita ni kuchelewa.
Umri sio kigezo cha kutofanikiwa, sio kigezo cha kutofanya mambo makubwa.
See you at the top
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476/ 0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com
Edius Bide Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476/ 0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com
Usisite kulike page yetu ya facebook hapa chini.
Karibu kuweka oda ya kitabu cha "Barabara Ya Mafanikio".
Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment