Thursday, 22 June 2017

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba wewe u mzima wa afya na unaendelea vizuri na majukumu yako. 

Karibu tena katika makala nzuri ya Leo niliyokuandalia. Natumaini hupo tayari kujifunza kwani kuna msemo unasema "mwanafunzi akiwa tayari, mwalimu hutokeza."
Kitu kimojawapo ambacho kitakusaidia kujifunza au kupata maelekezo au mafunzo yoyote kwa haraka ni kuuliza. 
                                  

Kuuliza ni njia rahisi na ya haraka itakayokusaidia kujifunza.  Mara nyingi nimekuwa nikijitahidi kujifunza kwa kuuliza na katika kuuliza nimepata kujua mambo mengi. 

Kuna wakati unaweza kuwa  unakwenda mahali sehemu fulani umeelekezwa kwa juu juu tu na mtu unayekwenda kwake, hivyo ukiwa njiani unatembea kwa kujiamini kabisa kwamba Huwezi kupotea. Kila unayekutana naye njiani hata hujisumbui kumuuliza ni njia ipi itakayokufikisha mahali unakokwenda. Baada ya kutembea umbali mrefu unashtuka umepotea njia ndipo unapoanza kuuliza watu. "Hivi kwa mtu fulani ni wapi? " wanakuelekeza na unaweza kufika kiurahisi. Kumbuka umepoteza nguvu nyingi na pia muda mwingi njiani kumbe ungeacha kujifanya mjuaji ungelifika haraka unakokwenda. 


Hivyi ndivyo maisha yetu tunapaswa kuyajenga kwa kujitahidi kujifunza kwa kuuliza na hii ni njia rahisi ya kuyafikia mafanikio unayoyataka.
Kuna methali ya kiswahili inasema "Kuuliza si ujinga." kumbe unapouliza unatoa ujinga na kujiingizia maarifa. Warren Buffet  ambaye ni tajiri namba 3 duniani  aliwahi kusema "if you learn you earn. " akimaanisha "kama ukijifunza, unajiweka katika wakati mzuri wa kupata pesa. "

Kuhusu kuuliza wachina wana msemo unaosema "ni bora kuuliza swali na uonekane mpumbavu dakika 5, kuliko kutokuuliza na ubaki mpumbavu maisha yako yote. " Nakumbuka kabla sijaanza kuandika kitabu changu cha Barabara ya mafanikio, nilimuuliza Kaka Lazaro Samwel (Mwandishi wa kitabu cha Nguzo tatu za maisha)  namna ya kuandika kitabu na yeye alikuwa tayari kunifundisha. Ilikuwa kazi rahisi sana kwangu baada ya hapo niliweza kuandika kitabu hicho. 


Jifunze kuuliza itakusaidia lakini kumbuka pia kuuliza watu sahii na unaowaamini. 

Mafanikio yapo mikononi mwako.

Ndimi
Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya facebook hapa chini (bideism blog). 

Karibu pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri cha Barabara Ya Mafanikio kwa mawasiliano yangu hapo juu.

Washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: