Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG. Ni matumaini yangu kwamba umeamka
salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu
yako ya leo. Tumshukuru Mungu kwa kutupa siku nzuri kama ya leo. Leo ni
siku muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow.
Karibu sana katika Makala ya leo
niliyokuandalia.
Wakati anaandika kitabu chake cha
NGUZO TATU ZA MAISHA, Mwandishi Lazaro Samwel aliweka mahusiano, kama nguzo
mojawapo ya maisha, ukiachana na maendeleo binafsi na ujasiriamali. Ni
mwandishi mzuri sana katika tasnia ya uandishi, ukisoma maandiko yake
utakubaliana na kile ninachokisema.
Kwenye kitabu hiki, cha Nguzo Tatu Za
Maisha, kuhusu mahusiano nimeona maneno matatu muhimu kwenye mahusiano ambayo
yatakusaidia kwenye mahusiano yoyote uliyomo, maneno hayo ni:
a)
Asante:
Asante ni neno dogo lenye herufi sita
lakini lina maana kubwa sana kwa mtu ambaye uko naye kwenye mahusiano. Neno ili
sit u muhimu kwa watu waliokwenye mahusiano au ndoa, ni neno muhimu kwa mtu
yeyoyote kwenye jamii. Unapofanyiwa jambo la ukarimu, jifunze kesema asante,
mtu aliyekufanyia kitendo hicho ataona unathamini jambo alilolitenda na ataona
kwamba unamthamini pia. Ukiletewa zawadi, ukifanyiwa ukarimu, sema “Asante.’’
Jifunze ata kujishukuru mwenyewe, kwa kusema asante, ata pale tu unapoamka
kitandani, unapokwenda kuoga, kuna kitu kipya utakiona kama mabadiliko kwenye
maisha yako. Neno asante ni dogo lakini wengi linawashinda kutamka. Nakumbuka
tukiwa wadogo, mama alikuwa akikuletea zawadi kama vile nguo, usiposema asante,
zawadi hiyo ulikuwa ukinyan’ganywa. Ilikua ni njia nzuri ya kutufundisha
kushukuru.
b)
Hongera:
Jifunze kumpongeza mwenzako kwa kila
jambo zuri analolifanya. Hii itampa motisha kwa kuzidi kusonga mbele kwenye
mafanikio na maisha yake kwa ujumla. Hakuna kitu kibaya kama kufanya jambo zuri
alafu mtu wako wa karibu hasikupe pongezi, inakatisha tamaa kwa kiasi Fulani.
Mtu uliyenaye kwenye mahusiano, akivaa vizuri mwambie “hongera umependeza.”
Akifanya vizuri kwenye kitu fulani mwambie “Hongera” hata kama ni jambo dogo.
c)
Samahani
Neno
“samahani” ni neno dogo lakini
limesababisha mahusiano mengi kuvunjika na kuishia pabaya kwa watu kushindwa
kukiri makosa na kuomba msamaha. Watu wote sio wakamilifu, kukosea kupo tu.
Jifunze kusamehe hata kama hujaombwa msamaha. Samehe kila siku kabla ujalala
kwani kutunza kinyongo na hasira juu ya mtu ambaye huko naye kwenye mahusiano
ni kumkaribisha shetani kuyaingilia mahusiano yenu. Kumbuka mazuri yote ambayo
uliwahi kufanyiwa yanazidi kosa moja tu ulilotendewa,\. Jifunze kukiri makosa
na kusema “samahani” kwa mtu uliyemkosea hata kama umefanya kosa dogo namna
gani. John Billings aliwahi kusema “Hakuna kisasi kilichokamilika kama
msamaha.” Kumbe ukitaka kulipiza kisasi kikubwa toa msamaha. Wengine wamekuwa
wakiwaza kwamba kuomba msamaha ni kujishusha, lakini hayo ni mawazo mgando
(stinking thinking). Jifunze kuomba msamaha kwa kusema “samahani” itakusaidia. “Unforgiveness blocks blessings;
forgiveness releases blessings” anasema John Mason mwandishi
maarufu wa vitabu vinavyohusu huamasishaji akimaanisha “kutosamehe huondoa Baraka; kusamehe
huleta Baraka.”
Nakutakia
utekelezaji mwema.
SEE YOU AT THE TOP
Ndimi
Edius bide katamugora
Author and motivational speaker
0764145476/ 0625951842
Email:
ekatamugora@gmail.com
Kwa
atakaye hitaji kitabu cha Nguzo Tatu Za Maisha anaweza kuwasilaiana nami
kupitia namba zilizowekwa hapo juu.
Karibu
pia kuweka oda ya kitabu changu kizuri kinachozungumzia mengi kuhusu mafanikio
kinachoitwa BARABARA YA MAFANIKIO (Mafanikio
yako mikononi mwako).
Washirikishe na wenzako ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment