Mjuaji ni mtu
anayejifanya kujua kila jambo. Mara nyingi
ukikutana naye atakwambia jambo hili alifanywi hivi linafanywa hivi au
hacha kufanya hivi fanya namna hii.
Wafanyaji ni wale watu wanaofanya mambo
yanayoonekana, hawa si wababaishaji.
Mara nyingi ukiwa unafanya kitu ambacho unaamini ni
ndoto yako wajuaji watakao kujia ni wengi. Watakuja wakikwambia fanya hivi,
lakini wao hawajawahi hata kufanya kile unachokifanya au watakuja wakisema,
huwa wanafanya hivi na hawafanyi vile lakini ukiwauliza swali dogo tu kama hili
“ Umewahi kufanya kitu kama hiki?” utaona wanaanza kupepesa maneno, wakisema
mara ohoh niliwahi kuona mahali au huwaa wanafanya hivi. Ukiona au kukutana na
watu wa namna hii ttambua hawakufahi, waepuke kama ukoma tena sio wa kukaa
karibu nao.
Anza kutembea na
wafanyaji. Tafuta marafiki wanaofanya kitu kama wewe unachokifanys. Tafuta watu
waliowahi kufanya kitu unachokifanya maana wanajua changamoto ambazo
wanakumbana nazo na jinsi ya kuzitatua.
Wafanyaji ni kama
wachezaji na wajuaji ni kama mashabiki, mashabiki mara nyingi ujifanya wakijua
mpira Zaidi ya wachezaji wenyewe wanaokuwa uwanjani. Kuna msemo unasema, “Utamu
wa ngoma anaujua mchezaji na si mkaaji.” Mtu aliyekaa chini hawezi kuelezea
ngoma ilivyokolea kama yule anayeicheza. Hapa tunaweza kumfananisha mkaaji kama
mjuaji na yule anayecheza ngoma kama
mfanyaji.
Kumbe tuachane na
kuandamana na wajuaji tuanze kutembea na wafanyaji, kama ni biashara tafuta
mawazo na ushauri kwa watu wanaofanya biashara kama yako au tafuta watu wenye
ufahamu kuhusu biashara husika. Kama ni masomo
tafuta mtu aliyesoma masomo husika au mwenye ujuzi wa masomo husika,
ndiyo maama hata kidato cha tano na sita mwanafunzi wa masomo ya Sanaa anafundishwa
na mwalimu wa masomo ya Sanaa, na mwanafunzi wa sayansi anafundishwa na mwalimu
wa sayansi. Huwezi kuugua na kwenda kwa injinia akuandikie dawa ya kutumia,
lazima uende kwa daktari ndiye atakuandikia dawa sahihi. Lakini ukitaka ushauri
kuhusu nyumba yako lazima uende kwa injinia huwezi kwenda kwa daktari.
Wasikilize wafanyaji
usiwasikilize wajuaji. Achana na wajuaji, tembea na wafanyaji.
"Mafanikio Yapo Mikononi Mwako."
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com
Karibu ujipatie kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO, Kwa shilingi 6000/= mikoani tunatuma pia.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, washirikishe na wenzio kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment