Wednesday, 26 July 2017

Kusoma Kitabu Tena Sio Makosa

Habari mpendwa msomaji  wa  Bideism      Blog. 
Ni matumaini yangu kwambau mzima wa  afya.
Tumshukuru Mungu kwa siku Nzuri kama ya  Leo.Leo ni siku muhimu, usikubali ipotee. 
One day can make you grow. 
Karibu  sana katika Makala ya Leo 
niliyokuandalia.

Mara nyingi nimekuwa mpenzi wa kusoma vitabu na kusema ukweli vitabu vimenisaidia sana.
 Moja wapo ya njia nzuri ya kuongeza maarifa ni kusoma vitabu na maarifa yaliyo sahihi unaweza kuyapata kwenye vitabu.

Faida nyingine ya kusoma vitabu ni kwamba.   unaweza kupata maarifa ambayo ungeweza kuyatafuta kwa muda wa miaka 20 ukayapata ndani ya mwezi mmoja.
Mfano Napoleon Hill aliandika kitabu cha Think and grow rich baada ya uchunguzi wa miaka 25, ndipo alipoandika kitabu hicho. Huku akiwahoji matajiri 500 namna ya walioweza kupata mafanikio na utajiri wakiwemo Andrew Carnegie, Thomas Edson, Henry Ford, kutaja wachache. Kumbe ukisoma kitabu hicho unaweza kupata maarifa yaliyotafutwa ndani ya miaka 25 wewe ukayapata ndani ya wiki mbili, tena maarifa kutoka kwa watu 500.

Anthony Robbins ambaye ni mwandishi na mhamasishaji maarufu duniani yeye anasema kabla ya kufika umri wa miaka 19, tayari alikuwa amesoma vitabu zaidi ya 1000. Alisoma vitabu zaidi ya 700 ndani ya miaka 7. Kutoka na tabia ya kusoma vitabu imemsaidia kumjenga na kumpatia mafanikio makubwa sana, mbali na uhamasishaji amekuwa mshauri wa serikali nyingi duniani. 

Watu wengi waliofanikiwa wanasema vitabu, wewe mwenzangu unasubiri nini?, hata kama hupendi jitahidi uanze kidogo kidogo baadaye utazoea. Wachina wanasema "Safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja." Bill Gates, Warren Buffet na Oprah Winfrey wanajulikana kwa kuwa watu wanaopenda kusoma sana vitabu.

Kwa wale wanaopenda kusoma vitabu kama Mimi kuna wakati unaweza kubaki mpweke huku unatizama na kusema vitabu nilivyonavyo kwenye maktaba yangu tayari nimekwisha visoma vyote lakini kumbe kurudia kusoma vitabu sio kosa.

Jambo nililoligundua, ukirudia kusoma kitabu kuna mambo ambayo ulipokuwa unasoma ukayatilia maanani  kumbe ukisoma tena unaweza kuyapata tena na yakakusaidia sana.

Oprah Winfrey anasema yeye alisoma kitabu cha Think and grow rich cha Napoleon Hill mara 13 kabla ya kupata mafanikio aliyonayo sasa hivi. Kumbe kurudia kusoma kitabu ulichowahi kukisoma sio kosa hata kidogo.


"Mafanikio Yapo Mikononi Mwako."
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
AUTHOR AND MOTIVATIONAL SPEAKER
0764145476
0625951842
Email: ekatamugora@gmail.com
Karibu ujipatie kitabu changu cha BARABARA YA MAFANIKIO, Kwa shilingi 6000/= mikoani tunatuma pia.
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, washirikishe na wenzio kile ulichojifunza. 

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: