Sunday, 9 July 2017

Mambo Manne(4) Muhimu Ya Kufahamu Leo

Yafahamu mambo manne yatakayokupa motisha na kukuamsha kufikia mafanikio unayoyataka siku ya Leo.

==> Ulizaliwa kwa kusudi maalumu. Mungu amekuumba ili uje kutimiza kusudi Fulani. Haijalishi ulizaliwa katika mazingira gani. Mungu aumbi mitumba, Mungu aumbi vitu vya ovyo ovyo. Wewe ni tunda zuri LA uumbaji wa Mungu.

==> Umezaliwa mshindi kwani wakati unatungwa mimba, ulishindana na watu zaidi ya milioni thelathini (30), lakini ulipatikana na ukazaliwa wewe. Wewe ni mshindi.

==> Kila mtu anakitu cha tofauti ndani yake. Hakuna anayeweza kuandika kitabu kizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kuimba vizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kuhamasisha vizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kupiga vizuri ala za muziki kama wewe. Hakuna anayeweza kucheza mpira vizuri uwajani kama wewe. Hakuna anayeweza kuhubiri vizuri kama wewe. Hakuna anayeweza kuanzisha kampuni yenye brand nzuri na kubwa kama wewe. Anza sawa kufanya maajabu. Wewe ni wa pekee. Wewe ni special.

==> Usisubiri watu wengine waje kukwambia unaweza, anza wewe kujiambia kwamba unaweza. Isikilize ile sauti iliyo ndani mwako inayokwambia kwamba unaweza. Ukisubiri watu wengine waje kukwambia kwamba unaweza utachelewa sana. Mafanikio daima uanza na wewe. Mafanikio yapo mikononi mwako.

See you at the top

Ndimi
Edius Katamugora (Bide)
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email; ekatamugora@gmail.com

Kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio sasa kinapatikana kwa mawasilino niliyotoa hapo juu.

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana, washirikishe na wenzako kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: