Tuesday, 22 August 2017

Kuna Uzuri Katika Ubaya Wako

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo.
Tumshukuru Mungu kwa kutujalia siku nzuri kama ya Leo. Leo ni Siku muhimu, usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika makala ya leo niyokuandalia.

Watu wengi wamekua wakijidharau na kujishusha kutokana na madhaifu waliyonayo. Wamekuwa wakijiona hawafahi kuishi katika dunia hii kwani wanaona duniani si mahali sahihi. Lakini hawajui na hawafahamu kwamba wameumbwa ili kutimiza kusudi Fulani.

Leo hii nataka tutafakari kidogo kuhusu uzuri ulionao na kuachana na ubaya ambao wewe unauona. Hata kama kuna watu wanakudharau na kukuona haufahi lakini kuna kitu kikubwa ambacho umebeba wewe, ukikifanya dunia nzima itakuona wa ajabu na utabeba ushindi mkubwa.

Wakati natafakari kuhusu uzuri wa mtu, nimeona ni vyema niongelee mifano ya watu Fulani ambao unaweza kuwa unawafahamu au wengine hawafahau.

Helen Keller; mwanamama huyu alizaliwa akiwa anaona vizuri na macho yake mawili lakini alipofikia umri wa miaka miwili alipata ugonjwa mbaya uliompelekea kuwa kipofu wa maisha. Kuwa kipofu haikuwa mwisho wa maisha yake kwani akiwahi kusema, "Bora kuwa kipofu wa macho, kuliko kuwa kipofu wa maono." Hellen Keller pamoja na kuwa kipofu aliweza kusoma na kumaliza chuo kikuu na kupata kutunukiwa shahada ya sanaa. Huyu ni mtu, ambaye kwa mazingira yetu angelikua ombaomba lakini kwake haikua hivyo. Pamoja na hayo hakuishia hapo. Helen Keller amekuwa mwandishi mzuri na mhamasishaji na ni moja kati ya waandishi maarufu wa karne ya ishirini. Usijidharau rafiki yangu, kutokana na mapungufu yako unaweza kufanya makubwa.

Nick Vujicic; Huyu alizaliwa njiti ni mfupi kuliko kawaida. Ni RAIA wa Australia. Ufupi wake na yeye kuwa njiti hakukumfanya aishi maisha magumu. Amesoma na Leo hii ni mwandishi wa Vitabu na mhamasishaji mkubwa. Amekuwa akiwahamasisha watu kutokana na maisha yao. Ukimuona tu lazima useme Mimi nimekamilika na kumbe nahitaji kufanya kitu. Ili kuhamashisha watu lazima apande kwenye meza. Miguu yake ipo mifupi mno mithili ya mokono, amakweli tembea utaona mengi. Ameandika kitabu anachokiita "Life without limit." Yaani maisha  yasiyo na ukinzani. Tembelea mtandao wa YouTube umuone anavyofanya maajabu. Nick ameoa na tayari ana mtoto.Usijidharau kuna uzuri katika ubaya wako.
                             

Unaweza ukawa unajidharau kwa kitu ambacho umezaliwa nacho lakini kama ungelijua ungekitumia kitu hicho kama fursa. 
Siandiki maneno haya kama maneno ya kufurahisha lakini kuna watu wametumia madhaifu au ubaya wao kuwa fursa na wanatengeneza pesa kubwa sana. Nchi Uganda, mwanaume ambaye anasifika kuwa mbaya nchi nzima amechukua fursa hiyo na kuanza kuimba, video zake zinapendwa na kutazamwa sana sababu kuu ni ubaya wake. Nadhani pia unawafahamu wale vijana wafupi wa Nigeria wanaogiza kwenye filamu mbalimbali. Maarufu kama Aki na Ukwa. Hawa wametengeneza pesa kubwa sana kutokana na kuigiza lakini wanapendwa sana kutokana na ufupi wao. Leo hii ni mabilione kutokana na kuigiza. Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Habari utamaduni na michezo wamejitahidi kuwaalika nchi lakini wameshindwa hii ni kwasababu tu wamefanyiwa booking nyingi katika nchi mbalimbali. Usijidharau kuna kitu kikubwa ambacho wewe umekibeba na unaweza kutumia ubaya wako kufanya mambo makubwa.


Usifikiri mambo hasi , fikiria mambo chanya muda wote. Kila ukiamka na kujitazama kwenye kioo jisemee "Mimi ni mzuri, nimebarikiwa. Mungu ameniumba kwa kusudi Fulani." Usijishushe kuna uzuri katika ubaya wako. Ukijiweza kulitambua hilo utafanya makubwa. Usijali watu wanasema nini juu yako. Ipo siku wataelewa.

Ningependa kumalizia na maisha ya mtu mmoja ambaye kwa sasa nafanya naye kazi. Yeye katika mkono wa kushoto hana vidole vinne, kipo kimoja tu cha dole gumba. Sijawahi kumuuliza amekuaje lakini mtu huyo ni seremala mzuri huwezi kuamini. Anashikilia msumali na kupigilia vizuri tu kwenye mbao kama walivyo mafundi seremala wengine. Kwanini bado unajidharau?.
Kumbuka kuna uzuri katika ubaya wako.

"Mafanikio yapo mikononi mwako."

Ndimi;
 Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook hapa chini.

Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na rafiki yako kile ulichojifunza.

Kitabu cha Barabara Ya Mafanikio Bado Kinapatikana. Bei 6000/=

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: