Mwaka 2010 wakati najiunga kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook mambo yake hayakuwa kama yalivyoleo.
Nakumbuka kulikuwa na kitufe cha like basi lakini Leo hii kuna vitufe vingi vimeongezeka ukichunguza wanaviita reaction.
Haikuwa hivyo tu hata "people you may know" (watu unaowafahamu) walikuwa wachache sana. Yaani unajikuta una marafiki ambao hata uwafahamu lakini hiyo ndiyo ilikuwa hali halisi. Watumiaji walikuwa wachache.
Leo hii mambo yamebadilika kwenye Facebook kuliko kawaida. Karibu kila mtu anatumia Facebook. Kila mwaka wanaweka vitu vya kuvutia wanaongeza vitu mbalimbali. Mara utakumbushwa post uliyoiandika miaka 3 iliyopita au picha uliyotuma mwaka Jana.
Wamefikia hadi hatua ya kutengeneza video za kakukumbusha ulikuwa rafiki na mtu fulani miaka kadhaa iliyopita. Ni video nzuri sana kama umewahi kuziona.
Nafikiri hiki ndicho kinachosababisha Facebook kubaki kuwa mtandao wa kijamii nambari moja.
Nafikiri hiki ndicho kinachosababisha Facebook kubaki kuwa mtandao wa kijamii nambari moja.
Turudi kuona mtandao wa WhatsApp ambao mwaka Jana na mwaka huu muonekano wake ni wa tofauti. Mwaka Jana (2016) kulikuwa na sehemu moja ya kuandika status yako ambayo ni sehemu unapoweka kivuli chako (Display Picture (Dp)), lakini Leo hii unaweza kuweka status jinsi utakavyo tena wameweza kuweka hadi nyimbo na watu wakiongea ndizo hizi utasikia mtu akisema "Nitumie." Utafikiri kakununulia MB!.
Kwanini nayasema haya?
Wakati wengi tunaendelea kufurahia maisha na kuona teknolojia ikitupa vitu tunavyovitaka sisi wenyewe hatukubali kubadilika. Teknolojia inabadilika sisi ni wale miaka nenda rudi.
Yaani kama ni mfanyakazi wa umma utendaji wako ni ule ule toka umeajiriwa mwaka 2012, kuchelewa kazini ni wewe, kuwahi kutoka kazini ni wewe. Kukosa kazini ni wewe na visababu visivyo na mbele wala nyuma. Mwezi haupiti bila kuumwa. Ukifika kazini ni kushika simu kuanza kufuatilia siasa na umbea. Bado sijaongelea muda wa chai ambao wewe unatoka nusu saa kabla na kurudi nusu saa baada ya muda tajwa. Kwanini haubadiliki?
Naongea na wewe mwanafunzi ambaye kusoma kwako ni kulekule kwa mazoea mpaka utangaziwe mtihani ndipo unakumbuka kuna mambo ya kusoma. Kama ni chuo basi kale ka msemo ka "Chuo ni bata." Unakatendea haki kweli kweli. Kwanza nani alikwambia chuo ni bata? (Hili nitaliongelea siku nyingine.) Kwanini hubadiliki lakini?
Je wewe mfanyabiashara, ambaye toka watu wanasoma kidato cha kwanza hadi Leo hii wanafanya mtihani wa kidato cha nne bado aina yako ya uuzaji ni ile ile. Hutaki kujifunza vitu vipya. Mambo yamebadilika kuna kuuza kwenye mitandao wewe wateja wakija kwenye biashara yako wanakukuta huko busy na simu utafikiri unafatilia taarifa za biashara kumbe unafatilia ugomvi wa kina flani. Ukiona mteja unatamani anachokihitaji kisiwepo ili useme "Hakipo." Aondoke mapema ili uendelea kuchezea simu yako.
Wewe ukisikia biashara za mtandao ndio kwanza unasema "Ayanihusu haya."
Wewe ukisikia biashara za mtandao ndio kwanza unasema "Ayanihusu haya."
Na je wewe mkulima kila mwaka unalima mazao hayaoti umeshatafuta suluhu au bado unapanda tu ukisema "Mungu muumba atajalia." Umesahau kwamba "Muumba ndiye anayeumbua."
Kumbe sisi pia tunahitaji kubadilika kila siku iitwayo Leo ili kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia katika karne ya ishirini na moja. Tunahitaji kubadilika kwenye namna yetu ya utendaji kazi. Kujifunza vitu vipya kwani usipotaka kujifunza utakosa vingi.
Wiki iliyopita nchi ya Singapore ilitangaza watu wake kuacha kununua magari ifikapo 2018 Februari mwaka. Hii ni kutoka na kukua kwa teknolojia nchini humo. Wahenga walisema "Ukistaajabu ya Musa utaona ya Filauni." Wengine wakesema "Lisemwalo lipo kama halipo basi linakuja."Tusiende mbali hapa kwetu Tanzania kwenye taasisi za umma watu wengi wametangaziwa kuwa na ujuzi wa komputya mfano madaktari na walimu ili mambo yote ya uendeshaji yaende sawia. Sasa wale madaktari wanaoona kompyuta haziwafai lolote kuna siku mtatolewa kazini bure, huo ni mfano wa kawaida tu nakupa.
Jumatano ya wiki iliyopita nikiwa natembea mtaa wa pili ambao ni mtaa mpya ambako nyumba zinajengwa (napenda kutembelea sehemu mbalimbali kwa huwa najifunza mambo mengi. Tembea uone.) Niligundua kwenye nyumba nyingi mpya za mtaa huo zina madirisha ya vioo na aluminum, tena wengine wamediriki kuweka frame za vyuma na wakaanza kuishi wakitegemea mbeleni wataweka vioo na madirisha ya Aluminium.
Akili yangu ikaenda mbali na kuwaza hivi fundi seremala wa madirisha ya mbao wanafanya nini kwa sasa? Nafikiri jibu unalo. Teknolojia nimeanza kuwafuta taratibu watu wa namna hii. Fundi seremala ambaye hayuko tayari kujifunza kutengeneza madirisha ya vioo na aluminum kuna siku atalala njaa kwa mtindo huu.
Nchini China kuna maroboti ambayo yanatumika hotelini kama wahudumu yaani unaliagiza roboti linakuletea msosi hapo hapo ulipo. Kumbuka roboti halihitaji mshahara. Halipati mimba kwamba likuwa na likizo ya kujifungua, haligomi eti likitaka malimbikizo ya mshahara. Hapo umesema naongelea China umesahau kuwa hata ATM ni roboti ambalo limewafanya watu wengi kukosa kazi za benki ili hali kuna watu wengi wanasoma taaluma zinazohusu mambo ya kibenki na kifedha.
Leo ni kuachie jukumu moja.
Chukua kalamu na karatasi andika ni teknolojia gani ambayo ukiipuuzia itakuja kukuumiza siku za mbeleni.
Chukua kalamu na karatasi andika ni teknolojia gani ambayo ukiipuuzia itakuja kukuumiza siku za mbeleni.
Anza kuanzia Leo hii kujifunza kadri uwezavyo ili uweze kwenda sambamba na teknolojia husika. Kumbuka dunia ya Leo inakimbia kuliko kawaida, ni dunia inayobadilika kila kukicha. Wakati wewe unatembea, kuna wengine wanakimbia lakini pia kuna wengine wanapaa.
Wachina wanasema "Muda wa kupanda miti ulikuwa miaka kumi iliyopita. Muda mwingine muafaka ni sasa." Anza Leo. Jiandae vizuri weka mipango lukuki ya kwenda na dunia hii inayobadilika kila Leo. Abraham Lincoln aliwahi kusema "Kama ningekuwa na masaa sita ya kunoa mti ningetumia masaa manne yakwanza kunoa shoka." Akitaka kuonesha ni kwa jinsi gani mtu unatakiwa kujiandaa. "Kujiandaa ni siri ya mafanikio. " anasema Dr. Fr. Faustin Kamugisha.
Mabadiliko ya teknolojia yakustue.
"Mafanikio yapo mikononi mwako."
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
E-mail: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
E-mail: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Imani yangu ni kwamba Mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako kile ulichojifunza.
Karibu kujipatia kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa bei ya shilingi 6000/= tu. Tuwasiliane 0764145476.
0 comments:
Post a Comment