Monday, 23 October 2017

Naipenda Jumatatu

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kutimiza majukumu yako ya Leo. Leo ni siku muhimu usikubali ipotee.
One day can make you grow.
                                 
Leo hii ikiwa ni siku ya kwanza ya wiki, Jumatatu. Siku ambayo watu wengi hawaipendi kabisa. Yaani wengi wanatamani siku hii isingelikuwepo.

Lakini mimi naipenda Jumatatu. Ni siku ambayo kwangu naona inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye maisha yangu.

Jumatatu Kwangu ni siku ambayo ninaamka na motisha ya kusema nitafanya mambo makubwa wiki hii.

Jumatatu ni siku ambayo naandika malengo yangu ya kutimiza wiki nzima.

Kwanini watu huichukia Jumatatu?

Ili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza Mara nyingi na hatimaye nimepata majibu niliyoyahitaji.

Mara nyingi ukichunguza watu hupenda siku za Jumamosi na Jumapili au wikiendi.

Siku za wikiendi watu wanazipenda kwasababu ni siku ambazo hawafanyi kazi.

Watu wengi huichukia Jumatatu kwasababu tu wanafanya kazi wasizozipenda. Kazi ambazo haziwapi furaha.

Mwaka 1987 baada ya kufanya uchunguzi ilionekana kwamba zaidi ya 27% ya Wamarekani walifanya kazi wasizozipenda.

Leo hii kiwango hiki kimepanda hadi kufikia 80%. Hii ni hali ya hatari. Hapo hatujaangalia nchi za Kiafrika kama Tanzania.

Dr. John Schindler mwandishi wa kitabu cha "How to live 365 days fully." Anasema "Watu wengi hufariki kuanzia saa 9 usiku kuamkia Jumatatu saa 1 asubuhi kwa magonjwa ya Presha na Msongo wa mawazo." Hii utokana na watu kuwaza kurudi kwenye kazi wanazozichukia, hivyo wakianza kuwaza presha zinawapanda na hatimaye hufariki dunia.

Kumbe kuendelea kuichukia Jumatatu ni kujitafutia kifo cha bure. Ni kujiua pia.

Ufanye nini siku ya Jumatatu ili kutenda kazi kwa ufanisi na furaha.

1. Andika vitu vitano unavyojivunia kwenye maisha yako kwenye notebook yako kisha visome kabla ya kwenda kazini. Mfano: Mimi Edius ni mwandishi mzuri.

2. Andika vitu vitano vinavyokupa furaha. Na hakikisha unavifanya walau kimoja kwa siku hiyo.

3. Soma maneno yenye motisha ya kukutia moyo wa kusonga mbele. Mfano Mimi ukutani Kwangu nimeandika "Time waits for no man." Nikimaanisha "muda haumsubiri mtu yoyote." na "Kuzaliwa maskini sio kosa lako. Kosa lako ni kufa maskini."

4. Soma vitabu vya motisha. Vitabu vya motisha (self help books) husaidia watu kufikiri tofauti na kuwa na mitazamo chanya. Kumbuka watu wasiopenda kazi zao mara nyingi huwa na mitizamo hasi. Hivyo hii itakujengea kuwa na mtizamo chanya. Soma vitabu kila unapoamka kabla ya kuingia kazini.

5. Tizama video za Motisha kupitia mtandao wa YouTube. Hapa ingia kwenye Chanel kama Goal cast na TED. Utajifunza mengi.

Mimi naipenda Jumatatu. Wewe je?

Nakutakia Jumatatu njema.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp).
ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu kwa namba 0764145476. Tunatuma mikoa yote.
Washirikishe na wenzako kile ulichojifunza kwani mafanikio ni kitu cha kushirikishana

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: