Watu waliofanikiwa ni watu wanaotumia sana vichwa vyao kufikiri kwa uwezo wa juu sana. Ni watu wanaoumiza sana vichwa vyao.
HENRY FORD aliwahi kusema "Kufikiri ni kazi ngumu ndiyo maana ni watu wachache hujihusha nayo." Kumbe
kama wewe hautaki kutumia kichwa chako kufikiri ni wazi kwamba
utapishana na barabara yako ya mafanikio. Wewe unakwenda mashariki,
mafanikio yanakwenda magharibi. Ni wazi kwamba utachukua muda mwingi
kufanikiwa.
Watu waliofanikiwa wanatabia zifuatazo zinazowawezesha kufanikiwa;
Wanawaza kwa kutumia picha kubwa;
Ukiwaza kwa kutumia picha ni sawa na kuitabiri kesho. Kuiona kesho wakati bado unaishi Leo. Watu waliofanikiwa wanajiona baada ya miaka 5 au kumi watakuwa wapi. Je wewe umewahi kujiuliza tarehe kama ya Leo mwakani utakua umepiga hatua gani? Au kwako kila siku ni bora liende?. Anza kufikiri kwa kutumia picha kubwa. (Thinking with a big picture).

Wanawaza mambo chanya;
Siku zote watu waliofanikiwa hufikiri mambo chanya muda wote. Sio watu wanaowaza au kufikiri mambo hasi. Fikra hasi zimewafanya watu wadumae. Fikra hasi zimewafanya watu wasipige hatua yeyote. Kuna usemi unasema "chochote unachokiwaza unaweza kukileta katika uhalisia." Kuna nguvu kubwa inayobeba maneno mawili baada ya maneno "Mimi nini....'' Watu waliofanikiwa hujinenea maneno mazuri mbele ya maneno " Mimi ni..". Je wewe unajinenea maneno gani kila siku? Au ndiyo umekazana "Mimi ni maskini." Mimi sina akili kutaja machache.

Leo hii kuwa mtu wa kuwaza mambo chanya. Hata maisha yakikupa ugumu wa namna gani ona mambo chanya. Kuna mtu aliwahi kusema "maisha yakikupa limau. Tengeneza juisi." Huyu ni mtu aliyeona mambo chanya katika matatizo.
Wanajifunza kila siku;
Ukitaka kuongeza fikra zako lazima uongeze maarifa. Na njia pekee ya kuongeza maarifa ni kuwa mtu wa kujifunza kila siku. Soma vitabu, makala, magazeti yenye mafunzo(sio ya udaku), jikutanishe na watu wenye maarifa. Tembele maeneo mapya. Hakikisha unakuwa mtu wa kujifunza kila siku iitwayo leo.

Wanaishi na watu wanaofikiri kama wao;
Waingereza wana methali nzuri isemayo "Ndege wenye mabawa yanayofanana huruka pamoja." Kumbe watu wenye fikra kubwa muda mwingi hujenga ukaribu. Wanakuwa marafiki na wanashirikishana fikra zao. Ukitaka kufanikiwa lazima ubadilishe mzunguko wako wa marafiki. Tafuta marafiki wenye tabia nzuri, tafuta marafiki wanaowaza mambo chanya. Achana na marafiki wanaokurudisha nyuma. Epuka sana watu wanaosema:
Hautafanikiwa.
Mbona Fulani alifanya akashindwa.
Hatuna muda.
Ndio lakini.....
Ni ngumu kufanyika.
Haiwezekani.
Watu wa dizaini hiyo sio watu wa kuambatana nao.

Watu waliofanikiwa wanawaza kibunifu;
Ukiwa mtu Mwenye fikra kubwa fikra zao zitakuwa za kibunifu. Ukweli ni kwamba watu wengi wanapenda watu wanaowaza kibunifu. Hivyo ukiwa mtu unayetumia muda mwingi kuwaza mambo mazuri ubunifu kwako litakuwa suala la kawaida na watu watajileta kwako tu kutokana na ubunifu unaouonesha.

Hizo ni baadhi tu za sifa za namna watu waliofanikiwa wanavyofikiri.
Tukutane kesho kwa mwendelezo wa makala hii.
Mafanikio yako mikononi mwako.
Ndimi
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842
Unaweza kuwashirikisha wengine pia.
0 comments:
Post a Comment