Tuesday, 5 December 2017

Mambo 5 Ya Kufanya Ili Kuendeleza Ujuzi Wako

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kwenda kutimiza majukumu yako ya Leo.
Ni jambo jema la kumshukuru Mungu kitujalia siku nzuri iitwayo Leo.

Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

                            

Karibu Leo hii tujifunze mambo matano muhimu unayohitaji ili kuendeleza na kukuza ujuzi wako;

1. Tumia muda mwingi kuangalia watu unaotaka kuwa kama wao;
Jambo hili litakusaidia kujua watu wenye ujuzi kama wako wanautumiaje na wanafanya nini hadi kufikia hapo walipo. Hii pia itaipelekea akili yako mtazamo chanya wa kusema "Kama Fulani kaweza, kwanini mimi pia nisiweze?"

Watu unaootaka kuwa kama waoo ni hamasa kubwa sana kwako. Kila siku ukiamka na kabla ya kulala tizama ni kwa namna gani wanavyofanya ili kuendeleza ujuzi wao. Ipo wazi kwamba mara nyingi vitu tunavyoviona tunaweza kuviweka katika matendo yetu.

Pili, ukipata nafasi ya kujikutanisha nao jitambulishe na waambie inatamani siku moja kuwa kama wao na waulize waliwezaje kufika hapo walipo, nao watakuwa tayari kukupatia siri ambazo kabla wewe hukuzijua.

2. Nunua notibuku.
Notibuku yako itakusaidia kuandika mawazo yako ya Leo, malengo yako ya kesho na vitu unavyojifunza sehemu mbalimbali. Jifunze kutembea na notibuku yako muda mwingi kwani unaweza kupata wazo lako njiani na kuliandika ambalo baadae litakusaidia kukuza ujuzi wako.

Msanii Eminem wa Marekani ni mmojawapo wa watu wanaotembea na notibuku zao muda mwingi huku akiandika mawazo yake mbalimbali. Leo hii hakikisha notibuku yako na kalamu viko na wewe muda wote. Vifanye kama pete na kidole, muda wote haviachani. Wewe pia hutakiwi kuiacha notibuku yako mbali.

3. Kubali kuwa mtu wa kuthubutu.
Watu wote unaowaona na kushangaa kwamba wamekuwa magwiju wa kutumia ujuzi fulani ni kwasababu tu waliamua kuthubutu. Ukiwa mtu wa kuthubutu sio rahisi kushindwa kwenye kutumia ujuzi wako.

Watu wanaothubutu ni watu wasioogopa kukosea. Kumbuka kwamba hofu ya kukosea imewafanya watu wengi kutimiza ndoto zao. Inawezekana wewe ni mmoja wao. Ipo wazi kwamba unapoanza kijifunza kutumia ujuzi Fulani utakosea mara nyingi lakini ni katika watu hujifunza na hatimaye kuwa magwiji wa kutumia ujuzi wao.

Je, unataka kuwa gwiji katika kutumia ujuzi wako? Jibu ni moja tu, kubali kuthubutu na siku zote jifunze kutokana na makosa.

Nakubaliana na Robert Kiyosaki mwandishi wa kitabu cha Rich Dad, Poor Dad aliyewahi kusema;
     "Sijawahi kukutana na mtoto anayeanza kujifunza kutembea na asianguke.
Sijawahi kukutana na mtu aliyewahi kupenda ambaye hajawahi kuumizwa katika mahusiano.
Sijawahi kukutana na mcheza gofu ambaye hajawahi kupoteza mpira wa gofu.
 Sijawahi kukutana na tajiri ambaye hajawahi kupoteza pesa."  
 Haya yote  aliyasema akitaka kuonesha kwamba ut uthubutu ni kitu muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.

4. Tumia walau dakika 15 kila siku kufanyia mazoezi ujuzi wako.
Watu wote unaowaona na kuwashangaa wamewezaje kuwa wabobezi katika kutumia ujuzi fulani wanasiri kubwa ya kufanya kila siku. Wewe pia unahitaji kufanya mazoezi. Ujuzi mara nyingi hufanyishwa kazi na ubongo hivyo unavyofanya kila siku wako pia unaongezeka kiuwezo katika kufanya kazi juu ya ujuzi fulani. 

Wataalamu wanasema unapojifunza ujuzi fulani mpya, ubongo wako hutengeneza seli mpya. Hivyo hauna budi kutumia kila siku kufanya kitu Fulani kinachohusiana na kukuza na kuendeleza ujuzi wako.

Mwanafalsafa Aristotle aliwahi kusema "Sisi ni kile tunachokirudia mara nyingi. Ugwiji sio tendo bali ni tabia." Kumbe tunahitaji kuwa na tabia ya kufanyia mazoezi ujuzi wetu kila siku. "Ukitaka kucheza zumari, sharti ucheze zumari." Anasisitiza Albert Einstein.

5. Chagua kujitesa zaidi ya starehe.
Kuna wakati unafika ambapo unajiona kana kwamba tayari umekwisha bobea katika kutumia ujuzi wako. Hapo akili yako inaweza kukurubuni na kukwambia "Pumzika usijichoshe unaweza tayari.' Ukisikia sauti kama hii ndani yako hakikisha unaizima mara moja isiendelee kukutawala. Hilo ni giza kinalokutoa kwenye mwanga.

Hivyo usikubali kustarehe kisa umefikia hatua fulani watu Sasa wananakusifia ndipo uanze kujiskia na kuacha ulivyokuwa ukifanya mwanzo. Linapokuja suala la kukuza na kuendeleza ujuzi wako, chagua kujitesa zaidi ya starehe.

Mafanikio yako, mikononi mwako.

Ndimi:
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000 tu. Piga 0764145476
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako kile ulichojifunza.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: