Mojawapo ya sifa kubwa za watu waliofanikiwa ni kuamka mapema.
Hili ni tendo ambalo hufanywa kila siku na haijalishi ni siku gani yaani siku za kawaida za juma na siku za mapumziko yaani wikiendi.
Hili ni tendo ambalo hufanywa kila siku na haijalishi ni siku gani yaani siku za kawaida za juma na siku za mapumziko yaani wikiendi.
Baada ya kufatilia na kuwa mmoja wa watu wanaotumia vyema asubuhi nimegundua kwamba kuamka asubuhi sana kuna miujiza mingi ambayo watu wengi wangeifahamu wangekuwa na mashindano ya kuamka mapema na si mashindano ya kuvuta blanketi wakati jua limekwisha chomoza.
Muda ambao watu wengi husisitiza kama muda wa kuamka ni saa kumi na moja alfajiri. Ingawa watu wengine wameweza kuamka hadi saa kumi usiku.
Inawezekana bado unajiuliza, je mimi ambaye huamka saa moja nitawezaje kuamka asubuhi yote hiyo na nitafanya nini nikiamka? Hii ni tabia ambayo unaweza kuijenga lakini unahitaji nidhamu ya hali ya juu. Na wataalamu wanasema tabia mpya hujengwa ndani ya siku thelathini (30) bila kukwepesha hata siku moja maisha yako yote yanaweza kuwa ya kuamka asubuhi saa kumi na moja alfajiri.
Lakini kumbuka kama nilivyotangulia kusema jambo hili linahitaji nidhamu ya hali ya juu sana na pia kujitoa. Yaani ukisema naamka, Amka kweli. Kwani ukilala na ndoto zako zinalala lakini ukiamka ndoto zako zinatimilizika. Ndoto zako unazifanya kuwa kweli.
Kwanini nasema Muujiza Wa Asubuhi?
Ukiwa mtu wa kuamka asubuhi na mapema maisha yako yatakuwa ya tofauti kabisa na mtu mwingine yeyote. Watu watabaki kukushangaa.
Ukiwa mtu wa kuamka asubuhi na mapema maisha yako yatakuwa ya tofauti kabisa na mtu mwingine yeyote. Watu watabaki kukushangaa.
Ukiwa mtu wa kuamka asubuhi na mapema utaweza kufanya mambo mengi ambayo wengine wanaona hayawezekaniki kufanyika. Nakubaliana na John Mason, mwandishi wa vitabu aliyewahi kusema "Lisilowezekana, linawezekana."
Kuna faida kubwa utazipata ukiwa mtu wa kuamka asubuhi na mapema.
Zifuatazo ni baadhi ya faida;
Zifuatazo ni baadhi ya faida;
Kwanza kabisa unapata muda wa kusali na kumshukuru Mungu ambaye amekuumba na kukufanya uendelee kuishi hapa duniani. Bila yeye wewe si lolote si chochote. "Anza siku yako kwa sala. Maliza siku yako kwa sala." Anatukumbusha Rick Warren mwandishi wa kitabu cha Maisha yanayoendeshwa na kusudi.
Pili, unapata muda wa kufanya tafakari binafsi (meditation).
Kila mtu anahitaji kufanya tafakari kwani huufanya ubongo kufanya kazi kwa kiwango cha juu sana. Tafakari pia hupunguza msongo wa mawazo. Watu wanaofanya tafakari mara nyingi ni watu ambao hawapati msongo wa mawazo mara kwa mara.
Kila mtu anahitaji kufanya tafakari kwani huufanya ubongo kufanya kazi kwa kiwango cha juu sana. Tafakari pia hupunguza msongo wa mawazo. Watu wanaofanya tafakari mara nyingi ni watu ambao hawapati msongo wa mawazo mara kwa mara.
Tafakari pia husaidia kumwonesha mtu amepiga hatua gani na ametimizaje malengo yake. Hapa mtu anaweza kufanya na kuweka malengo mapya.
Tatu, kuamka mapema kutakusaidia kupata muda wa kufanya mazoezi ya mwili. Mazoezi ni afya na husaidia kuuweka mwili katika hali safi na pia hupunguza msongo wa mawazo (Stress). Mazoezi pia huufanya ubongo uwe na nguvu na kufanya kazi kwa uwezo mkubwa sana. Usisubiri daktari akwambie anza kufanya mazoezi. Sio mpaka uandikiwe dozi ya mazoezi ndo uanze kuyafanya.
NNE: Kuamka mapema husaidia kupata muda wa kusoma vitabu mbalimbali na kuongeza maarifa. Wakati watu wanalalamika wamebanwa sana na hawapati muda wa kusoma vitabu, ukiwa mtu wa kuamka asubuhi na mapema kwako muda wa kusoma vitabu hauwezi kukosekana. Kumbuka pia watu waliofanikiwa ni wapenzi wa kusoma Vitabu na ni watu wanaopenda kujifunza na kutafuta maarifa. Je umekubali kuangamia kwa kukosa maarifa? Kusoma ndiyo njia mpya ya kuiweka aplikesheni mpya katika kichwa chako.
Tano, kupata muda wa ziada; ukiamka mapema unaweza kupata muda wa ziada wa kufanya mambo ambayo yapo nje ya kazi yako (hasa wale walioajiriwa) au shughuli zako za kila siku. Unaweza kufanya kazi zako kabla hakujakucha na baadaye ukaendelea na kazi zako za kiofisi.
Rafiki yangu mmoja ambaye ameniambia kwamba yeye siku hizi huamka saa kumi na kufanya mambo yote ambayo nimeyaorodhesha hapo juu. Yeye saa kumi na moja huelekea bustani kwake na kufanya shughuli za kibustani. Jua likichomoza anakuwa tayari akifanya shughuli zake za kijamii. Huyu anaonesha wazi hule msemo wa "Wote tumejaaliwa Massa ishirini na nne, lakini tofauti yetu huja kwenye matumizi." Unataka muda wa ziada? Anza Leo kuamka mapema na utaiona miujiza ya asubuhi.
Sita: hii ni kwa wanafunzi na wanaojiendeleza kitaaluma.
Baada ya timu ya uchunguzi na wataalamu kutoka chuo kikuu cha California, Berkeley nchini Marekani wakiongozwa na Dkt. Mathew Walket waligundua kwamba, muda wa asubuhi ubongo unakuwa kama sponji na hivyo kuweza kuweka mambo katika akili kwa wepesi zaidi yale unayokuwa ukiyasoma. Hivyo ukiutumia muda wa asubuhi kusoma unaweza kuelewa kwa kasi sana kuliko muda mwingine wowote. Huu nao ni miujiza wa asubuhi.
Baada ya timu ya uchunguzi na wataalamu kutoka chuo kikuu cha California, Berkeley nchini Marekani wakiongozwa na Dkt. Mathew Walket waligundua kwamba, muda wa asubuhi ubongo unakuwa kama sponji na hivyo kuweza kuweka mambo katika akili kwa wepesi zaidi yale unayokuwa ukiyasoma. Hivyo ukiutumia muda wa asubuhi kusoma unaweza kuelewa kwa kasi sana kuliko muda mwingine wowote. Huu nao ni miujiza wa asubuhi.
Ukitaka Leo kuamka kuifaidi miujiza hii ya asubuhi anza kuamka mapema. Ipo siku utakuwa mtu wa tofauti na watu wakikuuliza usisite kuwaambia kuwa siri kubwa ni miujiza ya asubuhi.
"Ewe mvivu, utalala hata lini?
Utaondoka lini katika usingizi wako?" -Biblia
"Mafanikio yako, mikononi mwako."
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Edius Katamugora
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram: ediuskatamugora
Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000 tu. Piga 0764145476
Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe na mwenzako kile ulichojifunza.
0 comments:
Post a Comment