Mwanzoni nilichukia sana mambo yanayohusu ujasiriamali na biashara. Hivyo nikawa najisemea mwenyewe "siwezi wala sina ndoto za kufanya biashara yoyote wala kujihusisha na mambo ya ujasiriamali." Baada ya kusoma vitabu vingi na kukua kifikra niligundua yakwamba huwezi kufanikiwa na kupata uhuru wa kifedha bila kufanya biashara au kuwa mjasiriamali.
Kabla ya kuwa mjasiriamali kuna mambo mengi unatakiwa kujifunza na kuyajua. Lakini mbali na kuwa na mambo mengi unayotakiwa kuyajua kuna mambo ya muhimu sana unatakiwa kuyafahamu kabla ya kufanya biashara au ujasiriamali.
(Kupata kitabu hiki Piga, 0764145476/0625951842)
Mambo hayo muhimu ni haya yafuatayo;
- 1. Jifunze kuwasiliana.
"Watu maskini ni watu wasiojua kuwasiliana." anasema Robert Kiyosaki mtunzi na Mwandishi maarufu wa kitabu cha Rich Dad, Poor Dad. Naye mhamasishaji Jim Rohn alikuwa na haya ya kusema "Wewe ni maskini kwasababu watu hawajui lolote kuhusu wewe." Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema "Wewe ni maskini kwasababu hauwezi kuwasiliana yale mazuri uliyonayo na watu wakaja kununua bidhaa yako."
Ukiweza kuwa mtu anayejua kuwasiliana vizuri na watu utaweza kufanya biashara yenye mafanikio makubwa na pia kuwa mjasiriamali anayefanikiwa sana. "Uwezo wako wa kuwasiliana na watu vizuri utachangia asilimia 85 ya mafanikio kwenye biashara na maisha yako." Anasema Brian Tracy mwandishi wa vitabu toka Marekani.
Uwezo wako wa kuwasiliana ndio utachangia kuwa na wateja wanaoipenda biashara yako. Ikumbukwe pia somo hili la kuwasiliana halifundishwi shuleni au vyuoni lakini ni kitu muhimu kwenye biashara yako na kwenye maisha yako kama una ndoto ya kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa sana.
Mambo yanayoweza kukusaidia kuwa mtu anayewasiliana vizuri.
1.) Ongea na watu wote kwa heshima na chunga sana kauli zako mbele za watu. "Unapofungua kinywa chako, unaiambia dunia wewe ni nani." Anasema Les Brown mhasishaji maarufu toka Marekani.
2) Jifunze kusifia.
Mtunzi na Mwandishi wa kitabu cha "How to win friends and influence people" Dale Carnegie anasema "Watu wanapenda kusifia, na ukiwa mtu wa kusifia watu lazima watakupenda." Jifunze toka Leo kuwasifia watu. Wakipendeza wasifie, wakifanya kazi nzuri wasifie. Wakipiga hatua fulani wasifie. Chochote kizuri mtu anachokifanya jitahidi kumpa sifa zake, lakini usitoe sifa za kinafiki.
3) Jitahidi kuondoa hofu ya kuongea mbele za watu.
Kila mtu aliyebobea kuongea mbele za watu naye alianza kwa kuwaogopa watu hivyo alichukua muda na kuua hofu ya kuongea mbele za watu na Leo hii anaweza kuongea bila hofu mbele za watu. Kumbe hata wewe unaweza kujifunza kuongea mbele ya watu bila kuwa na hofu. Njia rahisi ni kuongea mbele za marafiki zako kwa kuchangia hoja mbalimbali zinazozungumzwa na pale unapopata fursa ya kuongea usikubali ipotee.
Bofya hapa kusoma: Jinsi Ya Kuondoa Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Watu
Bofya hapa kusoma: Jinsi Ya Kuondoa Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Watu
- 2). Jifunze kuuza.
Hakuna biashara yoyote au ujasiriamali wowote usiohusu mauzo. Hata kama unatumia kipaji chako lazima ukioneshe ndipo watu watalipia gharama fulani.
Najua unaweza sema sina kitu cha kuuza au sina mpango wa kuanza kuuza kitu fulani Mimi lengo langu ni kuuza kitu fulani. Unapojifunza kuuza kubali kuanza kuuza kitu chochote ili mradi kuna mambo utakayojifunza unapokuwa unauza kitu hicho na hatimaye baadae unaweza kuutumia ujuzi ulioupata ukautumia katika biashara ya ndoto zako.
Unaweza pia kumsaidia ndugu yako, familia au rafiki yako kutangaza nakuuza bidhaa zake ili uweze kupata ujuzi wa kuuza. Mauzo mara nyingi huhusisha ushawishi. Hivyo ukijifunza kuuza ukiwa bado hujaanza biashara yako, baadae ukianza kujihusisha mwenyewe na biashara yako utakuwa na uwezo na nguvu kubwa ya ushawishi.
Aliko Dangote, Tajiri namba moja Afrika alianza kuuza pipi akiwa anasoma shule ya msingi. Leo hii ameweza kufanya biashara kubwa sana na kuwekeza maeneo mengi Afrika, ikiwemo Tanzania ambako anamiliki kiwanda cha kutengeneza saruji, Dangote Cement.
Warren Buffet ambaye kwasasa ni Tajiri namba 3 duniani alikuwa akiuza pipi katika udogo wake mlango hadi mlango na aina ya pipi zilizopendwa sana ndizo alizozifanya kipaumbele katika mauzo yake. Leo hii anatajwa kama mwekezaji namba moja duniani.
Jifunze Leo ujuzi wa kuuza ili baadae ukusaidie unapoamua kuwa mjasiriamali.
Jifunze Leo ujuzi wa kuuza ili baadae ukusaidie unapoamua kuwa mjasiriamali.
"Mafanikio yako, mikononi mwako."
Ndimi;
Edius Katamugora
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 {WhatsApp}
Email: ekatamugora@gmail.com
Mwandishi na mhamasishaji
0764145476
0625951842 {WhatsApp}
Email: ekatamugora@gmail.com
Jipatie kitabu changu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Piga 0764145476.
0 comments:
Post a Comment