NAMNA
YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO UNASOMA.
(
HOW TO BECOME AN EXPERT WHILE AT SCHOOL )
HAUHITAJI
KUSOMA CHUO FULANI ILI UWE MTAALAMU.
Kuna
watu wengi wanafikiri yakwamba ukisoma chuo Fulani tayari hiyo ni tiketi ya
kuwa mtaalamu. Kama wewe ni mmoja wapo jua kwamba unajidanganya mwenyewe.
· Kusoma chuo fulani
sio tija kwamba utakuwa mtaalamu.
Usijisifu kusoma chuo Fulani kisa umeambiwa kusoma chuo unachosoma kinatoa
wataalamu wakati wewe huweki juhudi zozote.
· Ni mara ngapi
umeona watu waliosoma vyuo vinavyosifika kutoa wataalamu wanakosa kazi? miaka
nenda rudi wanazunguka ofisi moja hadi nyingine wakitafuta kazi.
· Au ni mara
ngapi umesikia watu wakisema ukisoma shule fulani tayari umefaulu na unakuta
mtu alikuwa kipanga na bado anafeli?. Kumbe chuo unachosoma sio tija kwamba
utakuwa mtaalamu.
Wewe
unayesema sijui chuo unachosoma hakina jina, hiyo isiwe sababu ya kukosa
kuutafuta utaalamu. Kama unasema chuo chako hakina jina kuwa wa kwanza
kulijenga wewe pia na wenzako. Inabidi ifike hatua ujisemee mwenyewe maneno
haya: “KAMA WATU WOTE WATAACHA KUUTAFUTA UTAALAMU, MIMI NITAKUWA WA MWISHO.”
Usikae chini na kuanza kunungunika kwamba chuo
chenu hakina jina, juhudi zako na kujituma vinaweza kukufanya uwe mtaalamu
popote ulipo.
Mfano wa mzee wa hekima na kijana mmoja.
Katika
kijiji kimoja kulikuwepo na mzee mmoja aliyekuwa amejawa busara na hekima ya
ajabu. Wakijiji wote walipokuwa wakipata shida yoyote, walimfuata ili awasaidie
ni kwa namna gani wanaweza kupata fumbuzi za matatizo yao. Kwakuwa alikuwa mzee
wa hekima na busara basi watu wote pale kijijini walimpenda mzee yule.
Sikumoja
kijana mmoja alitaka kumjaribu mzee huyo kama kweli ana hekima au la. Basi
alichukua ndege mmoja mdogo na kumweka kiganjani kwake huku akiwa amemfungia
vyema kiganjani mwake. Alipofika kwa yule mzee mwenye busara alimuuliza swali
kama ndege yule yu hai au amekufa. Alitaka mzee akisema ndege yule yu hai basi
ambinye kiganjani mwake afe. Au mzee yule mwenye busara akisema ndege yule
amefariki basi kijana yule angemwachia apae juu hewani.
Mzee
yule mwenye busara na hekima alijibu hivi “Kijana wangu, uhai wa ndege huyo
humo mikononi mwako, unaweza kumbinya afe au kumwachia apae juu hewani abaki
akiwa hai.”
Hadithi
hii inatufundisha nini.
· Uwezo wa kuwa
wataalamu huko mikononi mwetu, yeyote anayeamua na kusema kuwa anataka kuwa
mtaalamu anaweza kuwa.
Jifunze
kuchimba almasi mahali ulipo. Inawezekana chuo unachokisoma unakiona hakiwezi
kukufanya mtaalamu lakini mimi leo nakwambia mahali popote unaweza kuwa
mtaalamu. Majani ya mahali ulipo yanaweza kuwa hayaonekani ya kijani kumbe ni
upofu wa macho yako.
Katika
bara la Afrika kuna mkulima mmoja aliyekuwa na shamba moja kubwa sana. Kufanya kilimo
kwake lilikuwa jambo linalompa furaha muda wake wote. Hakuwahi kukosa furaha
maisha yake yote. Siku mmoja mzee mwenye hekima alimtembelea na kumwelezea
kuhusu utajiri uliopo katika almasi. Mzee mwenye hekima alimwambia, “Kama
ungelikuwa na almasi inayolingana na ukubwa wa kidole gumba ungeweza kuumiliki
mji wako wote. Kama ungelikuwa na almasi inayoligangana na kiganja chako
ungeweza kumiliki nchi yako nzima.” Kisha mzee huyo aliondoka. Usiku huo
mkulima huyo hakulala. Furaha yake yote ilipotea kabisa.
Asubuhi
iliyofuata alichukua uamuzi wa kuuza shamba lake na kwenda kuitafuta almasi. Alitafuta
Afrika nzima hakufanikiwa. Alitafuta Ulaya nzimalakini wapi. Alipofika nchi ya
Uhispania alikuwa tayari maskini wa kiakili, kinguvu na kifedha. Alikuwa amevunjika
sana moyo hivyo alijirusha katika mto Barcelona na kujiua.
Nyumbani
alikouza shamba. Yule bwana aliyenunua shamba lake alikuwa akiwanywesha ngamia
maji kwenye kijito kilichopita kwenye shamba lake. Ndani ya kijito kile mwanga
wa jua ulimulika jiwe na kulifanya litoe miale mikali. Alifikiri na kusema
linaweza kuwa jiwe zuri kutumika kama pambo nyumbani kwake hivyo alilichukuwa
jiwe lile. Mchana hule yule mzee mwenye hekima alirudi na kuona jiwe lile. Aliuliza,
“Hafiz amerudi?” Yule mmiliki mpya wa shamba alijibu, “Hapana, kwanini
umeuliza?.” Mzee mwenye hekima alijibu na kusema “Kwasababu hiyo ni almasi,
ninaitambua pale tu ninapoiona kwa macho.” Yule mtu alijibu, hapana, ni jiwe tu
nililoliokota kwenye mto. Njoo ujionee kuna mengine mengi.” Walikwenda na
kuokota baadhi na kuyachukua kwa wataalamu wa madini. Waligundua ya kwamba
shamba lile lilikuwa limezungukwa na almasi.
Kuna
mambo mawili ya kujifunza hapa.
Moja,
fursa mara nyingi huwa ziko chini ya miguu yetu lakini tunakimbia na kwenda
kuzitafuta pengine. Tunachohitaji ni kuzitumia fursa hizo. Ukiwa chuo hiyo
tayari ni fursa hakikisha unaitumia fursa hiyo vizuri.
Mbili,
fursa ikishajitokeza na kuondoka haiwezi kuja kama ilivyokuwa mwanzoni. Tumia
vizuri fursa uliyonayo leo ya kuwa shuleni kuutafuata utaalamu.
TANGAZO:
Bado
naendelea kupokea oda za kitabu cha NAMNA YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO UNAASOMA.
Kitabu hicho kitapatikana kwa watu 100 wa kwanza walioweka oda kwa bei ya
punguzo shilingi 5000/= baada ya hapo bei itabadilika. Kitabu hicho
kitapatikana kwa njia ya softcopy (NAKALA TETE) hivyo kila mtu ataweza kukipata.
Unangoja nini wewe rafiki yangu? Weka oda yako sasa kupitia;
0764145476(SMS)
0625951842(WhatsApp)
“MAFANIKIO
YAKO, MIKONONI MWAKO.”
Ndimi;
EDIUS
KATAMUGORA
Mwandishi
na Mhamasishaji
0 comments:
Post a Comment