Kukosa uvumilivu ni kitu
kilichowafanya watu wengi kuukosa utaalamu. Watu wengi hukata tamaa ndani ya
muda mfupi kutokana na kupata matokeo ambayo hawakuyatarajia. Ili uwe mtaalamu
unahitaji kuwa na uvumilivu wa hali ya juu. Wataalamu si watu wanaofanana na
yule sungura aliyeshindwa kufikia mkungu wa ndizi na kuanza kusema, SIZITAKI
MBICHI HIZI. Hasha ni watu wasiokata tamaa, ni watu wanaojua kwamba nyakati
ngumu hazidumu bali watu wagumu ndio wanaodumu.
Maisha yetu ya kila siku yanahitaji
uvumilivu bila uvumilivu maisha hayaendi. Mbuyu tunaouona ukiwa mkubwa upo leo
kwasababu ya mbegu iliyoweza kuingia ardhini na kuvumilia shida zote kama
kukosa maji na mengineyo, mtoto anazaliwa kwasababu mama yake aliweza kuvumilia
na kuitunza mimba ndani ya miezi tisa. Bahari shwari haitoi wanamaji hodari.
Watu mashuhuri, hodari na hodari ni watu walioweza kuvumilia na hatimaye leo
tunawaona na muda mwingine kuwachukulia kama watu wa mfano.
Bwana mmoja alikuwa akimiliki mgodi wa
dhahabu, baada ya kuchimba kwa muda Fulani alishutuka baada ya kuona haoni
madini ya dhhabu tena. Hivyo aliamua kumuuzia kijana mmoja machachari. Kijana
huyo hakuwa kama vijana wengine. Aliamua kwenda na kuwatafuta wataalamu wa
madini waje kuchunguza eneo lile. Wataalamu wale walitoka na majibu kuwa ardhi
hile bado ilikuwa na dhahabu ya kutosha. Baada ya kuanza kuchimba futi tatu
kutoka bwana wa kwanza alipoachia, walikutana na bahari ya dhahabu.
Anafanikiwa
yule anayevumilia anashinda yule anayevumilia. Anakuwa mtaalamu yule
anayevumilia. “Mashindano ya mbio hashindi mwenye mbio.”
(Mhubiri 9:11)
TANGAZO
Weka Oda yako ya Kitabu cha NAMNA YA KUWA MTAALAMU UKIWA BADO UNASOMA. Watu 100 wa kwanza kuweka oda watajipatia kitabu hicho kwa shilingi 5000/= tu baada ya hapo kitapatikana kwa shilingi 10000/= Kitabu hicho kitapatikana kwa njia ya NAKALA TETE utatumiwa kwa njia ya barua pepe (email) yako. Wahi sasa nafasi ni chache.
"Mafanikio yako mikononi mwako."
Ndimi
EDIUS KATAMUGORA
Mwandishi na Mhamasishaji
0764145476
ekatamugora@gmail.com
0 comments:
Post a Comment