Friday 24 March 2017

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na hupo tayari kutimiza majukumu yako katika siku hii ya leo. Nikukumbushe yakwamba leo ni siku muhimu katika maisha yako. Usikubali ipotee. "One day can make you grow".
Karibu sana katika Makala yetu ya leo inayosema "Fanya tu". Kuna wakati huwa hujisikii kufanya lolote yaani unaamka mchovu mchovu, ubongo ns mwili wako vinakushawishi kwamba leo hatufanyi lolote. Na wewe unakuwa tayari kuyapokea yale ambayo ubongo na mwili wako vinakwambia.
Leo nataka nikwambie Fanya tu hata kama hujisikii kuifanya,_amka kitandani jiingize katika kazi husika ambayo wewe utakuwa unahisi kuwa mvivu katika kuifanya.
Kampuni ya NiKE ina motto nzuri inayosema "JUST DO IT" ambayo inashabihiana na kile ninachokisema cha kufanya tu. Kama wewe ni mkula unahisi uvivu katika kwenda shambani siku ya leo,nakushauri uchukue jembe na uende shambani,bora hata ulime sehemu kidogo lakini kuna kitu umekifanya siku ya leo,au huenda unataka uende shambani kwako kesho na kuanzia kesho mvua zikaanza kunyesha wiki nzima na kujikuta siku zote saba hujafanya lolote shambani kwako.
Ama wewe ni mwanafunzi unahisi uchovu na uvivu,hutaki kwenda darasani kusoma (prepo), huenda leo hii ukurasa wa Kitabu ambao ungelifungua na kusoma leo ndipo swali lenye maksi ishirini litatoka katika mtihani. Nakupa ushauri wa bure JUST DO IT.
Ama wewe ni daktari, unahisi umechoka hutaki kwenda ofisini,huenda leo ndiyo siku ambayo ungeepusha vifo vya watu wengi. Na ukiinde kuwahudumia leo utapata Neema na baraka nyingi. Nami nakusihi nenda ofisini uepushe vifo Vinci vya watu, uwaponye watu maumivu na majeraha yao.
   Pengine labda wewe ni mwalimu,unahisi umechoks sana pia siku ya leo, unajihisi huwezi kuingia darasani na kufundisha. Nakuomba uende darasani "JUST DO IT". Pengine labda leo ndiyo  siku ambayo utafundisha kitu ambacho kitatoka kwenye mtihani wa taifa na wanafunzi wako watafaulu vizuri kabisa na kupata alama nzuri (flying colours). Au leo ndiyo siku ambayo utaongea maneno ambayo yatabadilisha maisha ya wanafunzi unaowafundisha na watakukumbuka miaka yao yote ya maisha yao. Kumbuka hizo ni baraka pia.
        Kumbe jambo la msingi ninalotaka kusisitiza hapa ni hule moyo wa kufanya kitu hata kama hujisikii kukifanya. Jijengee "Kufanya tu" na baadaye itakusaidia sana katika maisha yako. Ukijijengea kanuni hii maisha yako yatakuwa mazuri na itakuwa tabia. Maana uchunguzi uliofanyika unaonesha kwamba mwanadamu hutengeneza tabia MPYA ndani ya siku thelathini(30).
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane:
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com
Usisahau kuandika email yako hapa chini ili upate Makala hizi moja kwa moja.
"See you at the top".
Karibu tena katika blog hii na usisite kumshirikisha na mwenzio. Asante.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: