Sunday 20 August 2017

Matatizo Si Tatizo: Matatizo Ni Daraja Na Padre Dkt Faustin Kamugisha

Je, kuna watu ambao hawana matatizo kabisa? Hawana shinikizo la damu.
Hawana wasiwasi, hofu, mashaka, shida, mateso na sononoke. Watu wa namna hii wapo makaburini. Wameshaiaga dunia.

Kama wewe bado unapumua kuwa na matatizo ni kanuni ya maisha. Lakini matatizo si tatizo.

                                             

Matatizo yanafanya tuwe na uzoefu na tukomae. "Kila, tatizo ni zawadi bila matatizo tusingekua," alisema Anthony  "Tony" Robbins (alizaliwa Februari 29, 1960) wa Marekani, mwandishi wa vitabu vya kutia matumaini na hamasa. Matatizo ni fursa ya kukua. Mtoto anapojifunza kusimama anaanguka mara nyingi lakini anakomaa. "Tatizo si kwamba kuna matatizo. Tatizo ni kutegemea vinginevyo na kufikiria kwamba kuwa na matatizo ni tatizo," alisema Theodore Isaac Rubin (alizaliwa April 11, 1923) mtunzi wa vitabu wa Marekani.

Maneno hayo hapo juu ni maneno ya  Fr. Faustin Mwikila Kamugisha aliyoyoaandika kwenye kitabu chake cha Matizo si tatizo: Matatizo ni Daraja. Ni kitabu kizuri kinachoelimisha na kufungua akili kuhusu namna tunavyoyatizama matatizo. Nililinunua kitabu hiki mwaka 2016 lakini sijawahi kuchoka kukisoma kwani kina mafundisho makubwa na mazuri sana hasa kwa karne hii ya Ishirini na moja.

Mwandishi wa kitabu hiki amebobea sana katika uandishi na ameandika vitabu vingi vikiwemo, hatupangi kushindwa tunashindwa kupanga, Umevaa miwani gani: maji yakimwagika yanazoleka, make the most of every opportunity, MAISHA NI MTIHANI, ANDIKA JINA LAKO VIZURI, NDOA NI MTIHANI na vingine vingi lakini Mimi nimebahatika kuvisoma hivyo.

Bofya Hapa Kusoma: ALICHOANDIKA Padre Dkt Faustin Kamugisha Mtunzi wa Kitabu Matatizo si Tatizo Kuhusu KITABU CHA YUSUFU NINA NDOTO 

Kwenye kitabu chake hiki cha Matatizo si tatizo: matatizo ni Daraja. Fr. Faustin ametoa maana 26 za matatizo ambazo ni;


Matatizo ni Alama ya Mkato si Nukta.

Matatizo ni Fursa zenye Miiba.

Matatizo ni Changamoto.

Matatizo ni Ufunguo wa Mafanikio.

Matatizo ni Giza La Kusaidia kuona nyota

Matatizo ni Mawe ya Kuvukia.

Matatizo ni Mtihani.

Matatizo ni Msalaba.

Matatizo ni Mawimbi Katika Bahari Ya Maisha.

Matatizo ni Mtazamo.

Matatizo ni Ujumbe.

Matatizo ni mwisho wa Sura na Si mwisho wa Kitabu.

Matatizo ni weusi Ulioko Nyuma Mbele ni Kweupe.

Matatizo ni Sumaku inayokuvuta Uwe karibu na Mungu.

Matatizo ni Mapito.

Matatizo ni Matuta Katika Barabara Kuu ya Maisha.

Matatizo ni Ufunuo wa Uwepo wa Mungu.

Matatizo ni Somo.

Matatizo ni masahihisho.

Matatizo ni Kitendawili cha Kubarikiwa.

Matatizo ni Ishara ya Uhai.

Matatizo ni Ijumaa Kuu Inayotangulia Jumapili ya Paska.

Matatizo ni Majaribu

Matatizo ni Kinga

Matatizo yana Suluhisho.

Hizo ndizo maana za matatizo anazozitoa mwandishi. Nakushauri utafute kitabu hicho ukisome ili upate kujifunza zaidi kwa undani kuhusu maana ishirini na sita nilizoziandika hapo juu. Kupata kitabu hicho unaweza kuwasiliana nami kupitia namba zangu hapa chini.

Kitabu hiki kinafaa kusomwa na watu wote bila kujali rika, kiwango cha elimu, cheo, hali ya uchumi,kabila au rangi. Hii ni kwa Sababu matatizo na changamoto havina mwenyewe; humkuta kila binadamu aliye bado hai hapa duniani.

Ndimi;
Edius Katamugora (Mwandishi Bora wa Vyuo Vikuu)
0764145476
0758594893 (WhatsApp)
ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: