Thursday 9 March 2017

KIKULACHO KINGUONI MWAKO

Habari za asubuhi mpendwa msomaji wa BIDEISM BLOG .Ni matumaini kwamba uameamka salama na leo ni zawadi nzui sana tuliyojaliwa na Mungu ambayo tukiitumia tutaweza kufanikiwa kikubwa zaidi.

Karibu sana katika makala ya leo inayosema ''KIKULACHO KINGUONI MWAKO''.
Ndugu mpendwa ni mara ngapi tumekuwa tukizilalamikia familia zetu,serikali,marafiki na jamii inayotuzunguka kwa ujumla kuhusu mafanikio yetu?. na kusahau ya kwamba sisi wenyewe ndio wenye majukumu makubwa na mafanikio yetu wenyewe ( we are responsible for our own success).

Leo nataka nikuweke wazi yakwamba, chawa,kunguni,viroboto,mba na vingine vingi vinavyokutafuna unavitengeneza wewe mwenyewe na si wazazi wako,serikali au jumuiya inayokuzunguka. Ukitaka kumuona mchawi wa mafanikio yako nenda kwenye kioo utamuona, uwiii sasa sijui utamuona nani zaidi yako.

Ndugu msomaji mara zote tutambue kuwa mafanikio yako mikononi mwetu kama sisi wenyewe tukiamua kubadilika na kujishughulisha na kuweka juhudi na bidii katika yale tunayoyafanya. Rafiki yangu ndugu GODIUS RWEYONGEZA mmiliki wa SONGAMBELE BLOG, aliwahi kuandika na kusema kuna watu tunazidiwa na viumbe visivyopewa uwezo wa kufikiri, imagine miti inauwezo wa kukua kufikia urefu wowote, sembuse wewe uliyezaliwa ukiwa na utashi na akili.

Kuna siku nilikuwa natizama maojiano kwenye Tv ambapo walikuwa wakimuhoji bwana WARREN BUFFET ambaye ni taajiri namba mbili duniani, aliulizwa swali ili, ''What is the greatest investment have you ever made?'', wakimaaanisha '' Ni uwekezaji gani mkubwa uliowahi kuufanya hadi leo hii'', naye akajibu ''The greatest investment i have ever made is investing in myself'' hapa alijibu akimaanisha '' Uwekezaji mkubwa niliowahi kuufanya ni kuwekeza katika mimi'. Mimi nilitegemea ataje labda biashara kubwa aliyowahi kuwekeza kwani tangu akiwa mtoto alikuwa akiuza pipi tofauti tofauti, nyumba hadi nyumba, mlango kwa mlango, pipi zilizonunuliwa sana ndizo aliendelea kuziuza. Tujifunze nini hapo, jambo la msingi kabisa ni sisi pia kuwa tayari kuwekeza katika sisi wenyewe, kwani mafanikio hayaji kama sisi wenyewe hatupo tayari kufanikiwa, muimbaji Farid Kubanda (FID Q_) aliwahi kuimba na kusema ''mabadiliko daima uanza na wewe'' kama haupo tayari kubadilika, hatu tukuombee mara ngapi utabaki palepale.

Wekeza katika wewe (invest in yourself), soma vitabu vitakusaidia kubadilika, kaa na marafiki wanawaza mafanikio na sio kula bada na kupiga stori zisizo na kichwa wala miguu, uzulia semina za uhamasishaji, angalia video YOUTUBE kama za kina ERIC SHIGONGO,MAKRITA AMANI, BISHOP T.D. JAKES, NICK VUJICIC,LES BROWN kutaja wachache nakuahidi mabadiliko makubwa. Weka bidii na juhudi katika kile unachokifanya kwani ''STRUGGLE IS A MOTHER OF SUCCESS'' ''Juhudi ni mama wa mafanikio, hakuna watu waliofanikiwa bila juhudi binafsi, mafanikio sio ajali, mafanikio sio bahati kama wengi wanavyofikiri.

Kumbuka: KIKULACHO KINGUONI MWAKO.

Ni mimi rafiki na ndugu yako.
EDIUS BIDE KATAMUGORA

Tuwasiliane:
0764145476
0625951842 (WHATSAPP).
Email: ekatamugora@gmail.com

'' See You At The Top''. 


Usisite kuwashirikisha wenzako kile ulichokipata hapa, na karibu tena kusoma makala nzuri kam hizi kwenye blog yako pendwa. Asante. 

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: