Wednesday 15 March 2017

Kuna Nini Katika Vitabu?





Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Nimatumaini yangu kwa umeamka salama na unaendelea vizuri kufanya kufanya kazi zako za kila siku. Nizidi tu kukumbusha kwamba leo ni siku muhimu sana kwenye maisha yako usikubalii ipotee. "One day can make you grow".
Karibu sana katika Makala ya leo "Kuna nini katika Vitabu?". Jana wakati nasoma historia ya Bill Gates tajiri namba moja duniani nilisoma yakwamba,alipenda sana kucheza na komputa na ilipofika miaka kumi na sita akawa kama ameathiriwa na kompyuta(addicted) ndipo wazazi wake walipo mkataza kujihusisha na mambo ya komputya kwani walihofia atafeli darasani. Bill Gates alikubaliana na matakwa ya wazazi wake na baadaye aliamua kujikita kusoma Vitabu. Hiki ndicho kilichonisukuma niandike Makala hii "kuna nini katika Vitabu?".
Ni Bill Gates huyu huyu ambaye kila mwaka anakuwa na likizo ya mwezi mmoja ambapo uchukua begi kubwa la Vitabu na likizo yake yote inaishia katika kusoma Vitabu?. Lakini pia Warren Buffet ambaye ni tajiri namba mbili duniani aliwahi kuulizwa ni uwekezaji mkubwa ambao hadi leo hii unajivunia naye akajibu "uwekezaji mkubwa ninao jivunia ni kuwekeza katika Mimi", akiendelea kusema kwa kusoma Vitabu.
Dr. Ben Carson kwenye Kitabu chake cha THINK BIG herufi "B" inasimama kueleze Vitabu na anasema   "ni katika Vitabu tunapokutana na watu wa zamani", Sikuishia hapo wakati nasoma Kitabu cha NGUZO 3 ZA MAISHA cha ndugu Lazaro Samwel, anasema "usijisumbue kuwaWekea watoto wako akiba katika benki,warithishe kusoma Vitabu". Bado nikaendelea kujiuliza "kuna nini katika Vitabu". Kila aliyefanikiwa ukimuuliza siri kubwa ya mafanikio hatakwambia ni Vitabu.
Kimsingi Vitabu vina majibu mengi ya matatizo yetu ya maisha tunayokimbana nayo. Ninapozungumzia Vitabu sizungumzii vile vya physics, historia wala jeografia hasha. Nazungumzia Vitabu vinavotia hamasa Vitabu vinavyoongelea maisha. Kuna Vitabu Vingi vinaongelea,muda,ndoa na mahusiano,pesa,utawala,biashara na ujasiramali,kutaja machache.
Binafsi baada ya kuanza kusoma Vitabu nimebadilika sana. Nakushauri na wewe rafiki yangu uanze kusoma Vitabu maisha yako yatabadilika naamini utanipenda.Kuna msemo wa kingereza unasema "five years from now will be determined by the books you read" yaani miaka mitano ijayo inatabiliwa na Vitabu unavyosoma. Anza leo kusoma Vitabu ubadili maisha yako. Anza kusoma Vitabu ufanikiwe. Kama ujui wapi pa kuanzia ni Vitabu gani usome tuwasiliane nipo tayari kukusaidia.
Ni mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane:
0764145476
0625951842(Whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com
"See you at the top"
Usisite kuwashirikisha wenzio kile unachokisoma hapa asante na Karibu.
Bideism: A mine of insights

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Unknown said...

Great job πŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌπŸ‘πŸΌ