Wednesday 29 March 2017

Mawazo Yanakuwa Vitu




Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba wewe rafiki yangu umeamka salama na umejiweka tayari kuhakikisha unanufaika na siku ya leo. Nidhidi tu kukumbusha kwamba leo ni siku muhimu usikubali ipotee hivi hivi. One day can make you grow
Karibu katika Makala ya leo inayosema " Mawazo huwa vitu". Thoughts become things. Hii ni ufupisho wa sheria ya asili kabisa iliyokuwepo toka enzi za mababu hadi leo hii. Toka kizazi cha kina Plato,Socrates, Edson, Ford,Roosevelt, hadi kina Steve Jobs, Bill Gates kutaja wachache. Sheria hii inajulikana kama sheria ya uvutano( The law of Attraction). Inayosema vitu vinavyofanana uvutana vyenyewe kwa vyenyewe ( Like attracts like).
Kwa undani sheria hii inazungumzia kwamba jinsi ulivyo leo ni kutokana na mawazo yako ya siku za nyuma. Ndiyo maana nikaipa Makala hii " Mawazo yanakuwa vitu". Ubongo na akili zetu ni kama sumaku kile tunachokiweka na kukifikiria Mara nyingi Mara kwa Mara ndicho kinachotokea kwenye maisha yetu.
Utabisha ya kwamba nimeandika uongo lakini ukweli utabaki kuwa hivyo. Ulivyo wewe leo ni kutokana na mawazo yako ya siku za nyuma. Mwandishi wa Kitabu cha " How to live 365 days" Dr. Sandler aliyefariki dunia mwaka 1957, anasema kati ya wagonjwa 4 waliolazwa kwenye vitanda vya hospitali watatu hawaumwi. Wanakuwa wanawaza kuumwa na hatimaye wanajikuta katika hali hiyo. Hii imewatokea wengi pale unsjihisi kuumwa ukienda hospitali kupima haoni lolote kwa maana kwamba huumwi. Ni kutokana na sheria hii ya uvutano. Unavyofikiri ndivyo unavyokuwa.
Kumbe mawazo yetu yanachangia kikubwa katika maisha yetu. Picha unayoiona leo kwenye maisha yako kuhusu kesho ndo hile hile itakayotokea. "Uzuri ni kwamba sheria hii haindani kabisa na muda inatupa muda wa kubadilisha picha zetu tunazoziona kila siku la sivyo maisha yangelikuwa magumu" anasema Lisa Nichols mwandishi wa Vitabu na muhamasishaji.
Jambo la msingi tunalopaswa kujifunza hapa kutokana na sheria hii ni kwamba inabidi tujenge picha chanya katika maisha yetu. Jinsi unavyojijengea picha chanya ndivyo akili yako inavyokusukuma kufanyia kazi picha unayoiona. Na jinsi unavyojijengea picha hasi ndivyo akili yako inavyokusukuma kuelekea mambo hasi. Ndiyo maana kuna watu walikuwa matajiri baadae wakafirisika na baadaye wakarudi kwenye utajiri wao wa zamani kwa sababu ya kutumia sheria hii. Raisi wa Marekani Bw. Trump ni mfano wa watumiaji wazuri wa kanuni hii aliwahi kufirisika miaka ya mwanzoni lakini baadae alirudisha utajiri wake.
Nawewe rafiki yangu nakusihi leo anza kutumia kanuni hii itakupa matokeo makubwa na naamini utanipenda. Kama leo umeamka na kusema "hii ni siku mbaya kwangu" badilisha sasa hivi na kusema " Leo ni siku nzuri sana kwangu, nitafanya makubwa". Fanya hivyo utaona maajabu makubwa. Kumbuka kama huna furaha ni kwasababu tu umekuwa ukiwaza mambo yasiyokuletea furaha. Na ujinga wa kuwaza mambo hasi ni kwamba ukiwaza jambo hasi moja mawazo mengine lukiki hasi yanajizakisha ( When you think of one negative thoughts other more negative thoughts do generate).
Ni Mimi rafiki na ndugu yako
Edius Bide Katamugora
Life Coach/Author/Motivation speaker.
0764145476
0625951842 ( Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com
Usisahau kutuma email yako hapa chini ili izipate Makala zangu moja kwa moja au tuma neno "Subscribe" kwenye namba ya whatsapp niliyoandika hapo juu niwe nakutumia Makala hizi.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: