Saturday 11 March 2017

Penye Miguu Mingi Ipo Njia

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na huko tayari kuitumikia kikamilifu siku ya Leo ili ikuletee maendeleo na mafanikio uweze kusonga mbele.

Karibu sana katika makala ya Leo "Penye miguu mingi,ipo njia".

NJIA ni mahari ambapo watu hupita. Pia ni namna au jinsi jambo fulani hufanyika. Naomba kwenye makala hii niunganishe maana hizi mbili ingawa nitakuwa na maana ya pili kitaswira zaidi.

Karibu katika harakati za kufikia mafanikio. Kuna njia nyingi za kufikia mafanikio. Watu tofauti hutumia njia tofauti kuelekea mafanikio. Waweza kutumia njia kama aliyotumia mwingine kufanikiwa na bado husifanikiwe au ukatumia na kufanikiwa.
Katika njia waweza kukuta alama tofauti za miguu ya watu tofauti tofauti wengine wakielekea uelekeapo na wengine kule utokako.

Kwa kawaida mahali ambapo hapakuwa na njia mwanzo pale wanapopita wengi mwisho njia huonekana/hutengenezeka.
Kuelekea mafanikio twaweza kutumia njia zaidi ya moja, waweza kutumia biashara, kilimo, teknolojia, au hata kiwanda, hizi zote ni njia. Lakini watu huogopa kupitia njia waliyopita watu wengi wakidhani hawataweza kufanikiwa kwa sababu wapo wengi. Kwa mfano biashara na ujasiriamali, wengi huogopa kuingia kupitia katika njia hizi wakidhani tayari wapo watu wengi( wanakwepa foreni).
Lakini pia Unaweza kupitia njia tofauti na Ile wanayotumia wengine na usifanikiwe. Nataka kukueleza pale penye miguu ya watu ipo NJIA. Pita mahala popote lakini kufanikiwa unahitaji kuwà "WEWE" ( Unique), kuwà na mtazamo na nidhamu tofauti wengine  hivyo utafanikiwa. Ni vyema kuwà na upekee katika kufanya kazi yako ili huonekane tofautii na Ile kazi yako iwe tofauti na ya wengine ( kuwà mbunifu). Ubunifu au creativity haufundishwi shuleni Bali ni wewe mwenyewe kucheza na akili yako.

Kuwà na muondoko tofauti na walio wengi ili uweze kufanikiwa. Kwa mfano mwaweza kuwà mnapita katika daraja bovu na mto chini kuna mto una kina kirefu cha maji. Kuvuka katika daraja hilo utahitaji kuwà makini na kuwà mbunifu na kuhesabu hatua zako ili uweze kuvuka bila kuanguka katika mto huo. Hesabu hatua zako za mafanikio ili uweze kufanikiwa na kufikia pale unapotaka kuwa. Kila la kheri katika safari ya mafanikio.


Makala hii imeandikwa na Evance Mujuni

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: