Monday 13 March 2017

We Are Equal But Not Equally Equal

Ni moja kati ya misemo ya Padre mmoja mwalimu Wangu wa sekondari iliyokuwa Ikinikosha sana. Huu msemo unamaanisha kuwa "Wanadamu  ni sawa lakini sio sawa sawia. Tunaweza kuwa tunatembea kwa miguu miwili, tunaona kwa macho Mawili na tunavuta hewa moja oxygen lakini Sisi sio sawa hata kidogo. Kila mwanadamu ni kiumbe tofauti na mwenzake na kila mmoja ana njia yake aliyopangiwa kimaisha.
Wengi wetu hupenda kupima mafanikio yetu kwa kujilinganisha na wenzetu wa umri sawa,kipato sawa,ukoo mmoja au hasa kiwango kimoja cha elimu.
Ukimuuliza leo kijana mdogo wa chuo mwaka wa kwanza kwamba anajiona wapi miaka kumi ijayo,Nina imani jibu litakuwa linaongelea maisha ya kitajiri,nyumba,mke au mume na watoto katika shule nzuri.
Hii ni ndoto ya kila kijana lakini muda huo wa miaka kumi unaweza kupita bila kutimiza ndoto zake. Hapo ndipo wengine hukata tamaa na kujiingiza katika mambo yasiyompendeza Mungu, ilimradi tu apate mafanikio ya haraka na kusahau kuwa riziki halali hutoka kwa Muumba.
Pamoja na kuwa bidii yetu na changamoto zetu ndizo zinatuwezesha au kutukwamisha kutimiza malengo yetu,tukumbuke daima kuwa sisi kama wanadamu hatuwezi kufanana kwa kila jambo. Kila mmoja wetu amepangiwa njia ya kupitia ili kukutana na riziki yake huko mbeleni mwa safari
Ninachotaka kukazia ni kwamba,tusipende kujilinganisha na wenzetu tunapopima mafanikio au maendeleo yetu. Watu wengine wanaweza kuwa mfano au "role models" kwa yale mazuri yao wanayoyatenda lakini wasiwe kipimo cha mafanikio yetu.
Trump ameingia madarakani uzeeni lakini Obama anastaafu akiwa bado na nguvu zake
Hawa ni watu wawili tofauti wamepata madaraka yaleyale lakini katika umri tofauti. Watu uliomaliza nao chuo wanaweza kupata ajira kabla yako haimaanishi watafanikiwa kabla yako. Wewe uliyechelewa kupata ajira unaweza kujiendeleza kimasomo na kuanziasha biashara na ukawaajiri haohao waliokutangulia.
Radio moja hapa nchini wanapenda kusema "usifosi tufanane", nami nawaachia neno hilo leo. Sisi tusilazimishe kufanana na wengine. Tumeumbwa na vipawa tofauti katika nyakati tofauti na mazingira tofauti. Kwa Marekani mwanafunzi bora ni yule mbunifu na mdadisi. Lakini kuna kukopiana na kutaka kujifananisha na wengine hatutaweza kufanikisha kutoka kimaisha. Tutabaki kuwaona na kuwaita "Freemasons" au wachawi. Ni ruksa kumuappriciate mtu lakini tusijifananishe Naye au kujipima mafanikio yetu kwa kumuangalia mwingine. Tuwe wabunifu na tunaotumia akili zetu sana. Mawazo ya wengine yana mchango pia lakini sisi mwisho wa siku ndio wenye maisha. Njia anazotumia A sio lazima mtu B akitumia atafanikiwa.
Mafanikio yetu yako mikononi mwa juhudi za kutekeleza mipango tunayojiwekea na sio watu tunaotaka kufanana nao au kuwazidi. Kuna mtu aliwahi kusema "comparison is always descriminative" kwa "kujilinganisha kunabagua".
Makala hii imeandikwa na :
EDGAR WILLIAM BUBERWA (0716116667)

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: