Monday 10 April 2017

Anza Siku Yako Ukiwa Na Furaha

Habari mpendwa msomaji wa makala za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari Leo kupambana kutimiza ndoto zako. Nikukumbushe kwamba Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika Makala ya Leo inayosema "anza siku yako kwa furaha.". Leo hii ni jumatatu ni siku ambayo watu wengi kwa uchunguzi wa kawaida wanaichukia. Ni siku isiyopendwa.  Mwanafunzi anawaza anarudi darasani kukutana na lile somo asilolipenda, mfanyakazi anawaza atakavyorudi kazini kwani anaona kazi abayoifanya haina maslai. Mfanyabiashara anarudi kweny biashara yake inayodilola siku hadi siku. Mwingine anatamani wikiendi iendelee azidi kula bata. Wakiyafikiria haya yote wanakosa furaha na kuichukia jumatatu. Utasikia wengi wakisema "It's a blue Monday."

Uchunguzi uliofanyika unaonesha kwamba wagonjwa wengi wenye matatizo ya moyo na presha ufariki usiku wa kuamkia jumatatu. Hii yote ni kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo na kuwaza jumatatu itakuwaje. Wanakosa furaha kabisa.

Leo nataka nikufundishe namna ya kuanza siku yako na furaha. Kwanza kabisa chukua kalamu na karatasi kisha orodhesha mambo yanayokupa wewe furaha, orodhesha mambo yanayokufanya wewe ujivunie kuwa wewe na jinsi ulivyo. Orodhesha mengi kadri uwezavyo. Kisha jaribu kuyasoma na kuyarudia kila Mara. Weka akili yako na mawazo yako kwenye mambo hayo. Kadri unavyojivutia kuwa na furaha na akili yako inajipa ruhusa ya kuwa na furaha. Anza leo kutumia njia hii utakuwa mtu Mwenye furaha muda wote.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145476
0625951842 (whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com

Usisahau kujiunga na mfumo wa email hapa chini ili upate Makala hizi kwenye email yako.

"See you at the top."

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments:

Unknown said...

I enjoy reading ur articles. You have a great talent, keep it up.