Saturday 15 April 2017

Jiepushe Na Watu Hawa

Habari mpendwa msomaji wa Makala hizi za Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na hupo tayari kwenda kutimiza majukumu yako kwa bidii na juhudi. Kumbuka Leo ni siku muhimu usikubali ipotee. One day can make you grow.

Karibu sana katika Makala yetu pendwa niliyokuandalia Leo hii.
Kuna wakati unakuwa na mawazo ambayo kwako wewe unazani ndiyo yale yaliyoyabeba kwa kiasi kikubwa mafanikio yako. Lakini unapoamua kuwaambia watu mawazo hayo uliyonayo watu hao wanakuwa na sababu milioni moja kwa nini wazo lako litashindwa.

Leo hii nataka nikwambie ya kwamba watu hawa au watu wa namna hii hawakufahi kabsa. Waepuke kadri uwezavyo, hata awe ndugu, mzazi au rafiki wa karibu kama anapoteza imani na wazo lako huyo hakufahi.

Hawa ni watu watakaokwambia kwamba mbona mtu Fulani alifanya kitu unachokifanya wewe na kushindwa. Ukichishikiza na watu hawa watakurudisha nyuma muda wowote. Hivyo ni bora ukaachana na kujitenga nao kabisa kwani hawachangii lolote katika kufanikiwa kwako Bali kupunguza imani yako juu ya wazo ulilonalo.

Chunguza leo watu unaoishi au kukaa nao muda mwingi. Je wanaimani na wazo lako. Kama hawana, wakimbie kabisa tena kwa spidi ya mwanga.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page yetu ya Facebook kwa kubofya page yetu hapa chini.

Usisahau pia kujiunga na mfumo wa email hapa chini ili uweze kupata Makala hizi.

"See you at the top"

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: