Thursday 6 April 2017

Kanuni Ya Dakika Mbili

Habari mpendwa msimaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka sawa katika kutimiza majukumu yako ya leo. Nikukumbushe yakwamba leo ni siku muhimu kwako usikubali ipotee. One day can make you grow.

Leo hii ningependa tujifunze kanuni moja muhimu sana inayoitwa "kanuni ya dakika mbili". Watu wengi tumekumbwa na tatizo la kuhairisha (procrastination) linalofanya mambo mengi yasifanikiwe. Ukitaka kufanya jambo Fulani unasita na kutoa mawazo Fulani ya kuacha kufanya kitu hicho. Mara sasa hivi kuna jua Kali nitafanya jioni au leo sio siku nzuri nitafanya kesho. Haya yote tukiendelea nayo tunakuwa tunashindwa kufanikiwa, tunajiwekea vikinzani dhidi ya mafanikio.

Kanuni ya dakika mbili inatumika au kufanya kazi hivi; chochote unachotaka kufanya kama kinauwezo wa kufanyika ndani ya dakika mbili wewe kifanye usikiache. Kama kufanya usafi mahali palipochafuka unaweza tumia dakika mbili Fanya usafi muda huu. Hii itakusaidia kuwa na matumizi mazuri ya muda na muda mwingine kukamilisha mambo kwa wakati.

Kanuni ya dakika mbili itakusaidia hata kuongeza utendaji na ufanisi wako kwani ukianza kitu utajikuta unatumia muda zaidi kukifanya. Mfano ni mara ngapi unasema ngoja niingie Whatsapp dakika mbili niangalie kilichopo au kwenye mtandao wa kijamii. Kinachotokea hapo unaweza kukuta umetumia  hadi lisaa lizima ukitumia simu yako wakati ulisema utatumia dakika mbili. Hivi ndivyo Kanuni hii inavyofanya kazi. Ukianza kitu utakifanya kwa muda wa ziada hata kama hukujisikia kukifanya. Mfano leo sema nitachukua Kitabu na kusoma ukurasa mmoja dakika mbili, utajikuta unasoma kurasa zaidi ya tano.

Nakushauri uanze leo kutumia kanuni hii na maisha yako yatabadilika.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Usisahau kulike page zetu hapa chini.

"See you at the top."

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: