Tuesday 18 April 2017

Mafanikio Ni Mazingira

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama.

Karibu sana katika makala ya leo. Hivi vinaweza kuwa vitu watu na wanyama. Kila mtu anaishi kwenye mazingira na mazingira yanachangia sana katika mafanikio ya mtu.

Kuna wakati utasikia, huyu anaongea kama watu wa sehemu Fulani au ana tabia kama za watu wa mahali Fulani. Kitu kinachosababisha watu waseme maneno hayo ni mazingira.

"Ukienda mahali wanapokula konokono na wewe utakula konokono tu"
Ni msemo wa Wahaya wa Tanzania. Kumbe jinsi tulivyo inategemea tumeishi au tunaishi mazingira gani. Tarehe 6 Agosti mwaka 1945 Marekani ilishusha mabomu mawili ya atomu katika maeneo ya Hiroshima na Nagasaki, mabomu hayo yalileta madhara makubwa ambayo baadae yalisababisha baadaye vianze kuzaliwa viumbe vya ajabu, unakuta mtoto anazaliwa bila kichwa wala miguu. Hii ilitokana na maeneo ya kukumbwa na janga lile.

Kuna hadithi moja ya tembo ambaye alikuwa akifugwa na binadamu tangu akiwa mdogo. Tembo huyo alikuwa akifungwa kwenye mti kama wanavyofungwa wanyama wengine kama mbuzi Kwa kutumia kamba hadi alipokuwa mkubwa. Tembo huyo aliendelea kufungwa mahali pale lakini hakutambua kuwa anaouwezo wa kutoka mahali pale alipofungwa na hakujua kwamba ananguvu nyingi mwilini mwake. Aliendelea kufungwa tu mahali pale.
   Hii ndiyo hali halisi ya mazingira tunayoishi Leo, mazingira ambayo wengi hatuyatambui, mazingira yaliyojaa wakatisha tamaa, yaliyojaa watu wasiopenda tufanikiwe. Jitahidi kusoma mazingira yako na kuyafikiria kwa makini ni ya namna gani. Inawezekana na wewe umefungwa kamba kama tembo na hujatambua kama unauwezo mkubwa. Kuna mtu aliwahi kusema "Jinsi ulivyo Leo na kesho ni matokeo ya Vitabu ulivyosoma na mazingira ul uliyoishi."

Ukiishi katika mazingira ya watu wasiojishughulisha na mambo ya dini utakuwa mpagani tu.
Ukiishi katika mazingira ya watu wasiopenda kufanya kazi utajikuta umetumbukia katika dimbwi la uzembe uliopindukia.
Ukiishi katika mazingira machafu utajikuta mchafu tu.
Ukiishi na watu wenye tabia mbovu na wewe utakuwa na tabia mbovu. Mazingira ni kipimo cha utu. Ni katika mazingira ambako tunafundishwa lugha na kuongea. Katika kujifunza kuongea tunajifunza kuwa na heshima kwa wakubwa ns hata wadogo, tunajifunza kuongea kwa busara, kwa unyenyekevu na Hekima. Haya yote ni matokeo ya mazingira.

Kama katika mazingira yako utafundishwa namna mbaya ya kuongea, uwezi kuonekana mtu mzuri Mbele za watu. Watu hatatakuwa tayari kukusikiliza na watapunguza heshima juu yako.
Ndio maana nasema mazingira ni mafanikio. Mazingira yetu ndio chachu kuu ya mafanikio. Mafanikio yamelala zaidi katika mazingira tunayoishi. Chagua Leo mazingira yapi ni bora ambayo ukiishi yatakupeleka kwenye mafanikio unayotamani kuyapata.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

1 comments: