Saturday 8 April 2017

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwa umeamka salama na hupo tayari kutimiza majukumu yako siku ya Leo. Nikukumbushe ya kwamba Leo ni siku muhumu sana katika maisha yako usikubali ipotee hivi hivi. One day can make you grow.

Karibu sana katika Makala ya Leo inayosema "weka alama". Tumekuwa na utamaduni wa kuwakumbuka watu muhimu kwenye historia Kama Jana ilivyokuwa kumbukumbu ya kifo cha Karume raisi wa kwanza wa Zanzibar. Hivi uliwahi kujiuliza kwanini tunafanya kumbukumbu za watu hawa. Jibu ni kwamba watu hawa waliacha alama(legacy) ambayo hatuwezi kuisahau. Mwalimu Nyerere na Karume walisaidia kuipatia nchi yetu Uhuru Leo hii Tanzania inaitwa nchi ya Amani. Ndiyo maana tunawakumbuka.

Watu wote mashuhuri duniani unaowasikia Leo hii.), watu kama, Steve Jobs, Mahatma Gandhi, Isaac Newton, Abraham Lincoln, Baraka Obama kutaja wachache wameweka alama mbalimbali ndiyo maana tunawakumbuka.

Kila mtu ameumbwa ili kutimiza kusudi Fulani ambalo ndilo lilimfanya Mungu atuumbe. Kila MTU ameumbwa kuweka alama (legacy) ambayo hakuna mtu atakaye kusaidia isipokuwa wewe. Kama ni kazini unakofanya kazi jiulize ukitoka Leo baada ya siku mbili au tatu mambo yataendaje?. Ukirudi na kusikia kila kitu kipo sawa tambua ya kwamba hakuna alama yeyote unayoiweka hapo. Ukiondoka na ukarudi na kusikia " mambo yalikuwa hayaendi ndugu kisa wewe kutikuwepo" hapo tambua ya kwamba kuna kitu ulichonacho ambacho bila wewe kuwepo hakifanyiki na hii ndiyo alama hasa.

Acha kufanya vitu kwa mazoea Fanya kwa bidii aswa ya juu kabisa watu waone umuhimu wako. Kama ni mtoto kwenye familia ukiondoka na kwenda mahali Fulani watu waumie na kusema kuna pengo umecha na sio waseme "ooh bora ameondoka" mtu wa hivi jua kwamba atimize kile anachokifanya.

Popote ulipo Leo hakikisha uwepo wako unaonekana. Watu waone umuhimu wako. Hilo ndilo kusudi la we we kuumbwa. Na furaha ya Mungu ni kuona wewe ukitimiza lengo lako.

Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email; ekatamugora@gmail.com

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: