Tuesday 4 April 2017

Wewe Sio Yule Wa Jana

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na umejiweka tayari kwenda kutimiza ndoto zako. Nikukumbushe tu kwamba leo ni siku muhimu kwako usikubali ipotee. " One day can make you grow."
Karibu sana katika Makala ya leo inayosema " Wewe sio yule wa Jana". Watu wengi wamekuwa wakiyashikisha au kuyahusisha maisha yao na Yale ya zamani. Kwa mfano mtu amekua katika familia isiyokuwa na maadili au maskini na kubaki mawazo yake yakimpelekea kwenye maisha yao ya zamani na kukubaliana na hali halisi.
Wanasaikolojia wanasema kwamba asilimia 85 ya familia zimejaa mikiki mikiki na sintofahamu za hapa na pale. Kwa hiyo kuwa na familia yenye matatizo ni jambo linalowakumba watu wengi sio wewe tu. " kuzaliwa maskini sio kosa lako kosa lako ni kufa maskini," anatukumbusha Bill Gates.
Kila mtu analalamika kuhusu maisha yake ya zamani utasikia, wazazi Wangu ni walevi, mama yangu alitelekezwa, naishi na mama wa kambo. Ni karibu stori ya kila mmoja watu. Sasa hapo unafanye?. Jambo la msingi kabisa ni kutambua kwamba wewe sio yule wa Jana na usiruhusu maisha yako yaendeshwe na Jana yako. Watu wengi wanabaki kulalamika juu ya wazazi wao, wengine hadi serikali lakini mafanikio yako mikononi mwako. Jiweke katika njia na lengo unayotaka kuwa pambana, weka juhudi na songa Mbele. Usikae chini na kulalamika tu bila kufanya lolote. " Nilizaliwa katika familia maskini, lakini niliichukulia kama changamoto," anasema Dkt. Legnard Mengi huyu utaona kwamba hakuendeshwa na maisha ya zamani.
'" MTU anayeielekeza akili na nawazo yake kwenye mambo mabaya yaliyotokea nyuma, anaombea kwa mabaya hayo hayo yatokee mbeleni. Kama huoni chochote na kusema nitakosa kitu Fulani siku zijazo, unasali na kuomba kukosa kitu hicho na kweli utakikosa." Anasema Prentice Mulford.
Amka leo pambana usiruhusu mawazo ya kizamani yaendeshe maisha yako. Weka uthubutu wa hali ya juu na utafanikiwa.
" You are not you're past."
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
0764145476
0625951842 (Whatsapp)
Email: ekatamugora
Usisahau kulike page zetu za Twitter, instagram na Facebook kwa kubofya link hapo chini.
"See you at the top."
Usisite kuwashirikisha wenzio kile ulichojifunza hapa.

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: