Saturday, 16 September 2017

Kilimo Ni Kazi Kama Zilivyo Kazi Nyingine

Kuna methali ya kiswahili inasema "Jembe halimtupi mkulima." Ikamaanisha ya kwamba mtu yeyote anayekubali kushika jembe na kwenda kulima lazima atapata mazao bora. Tena nikikumbuka lile shairi la "Karudi baba mmoja" aliwasisitiza wanawe kwamba mazao mazuri watayakuta shambani.
                                           
Kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa watu wanaofanya kilimo kuona kwamba kilimo sio kazi na kukichukulia kama kitu cha kupoteza muda.

Ukiwauliza wakulima "Unafanya kazi gani?" Wengi Watakijibu '' Sina kazi lakini najishughulisha na kilimo." Ukweli ni kwamba hamuitendei haki kazi yenu.

Kilimo ni kazi kama kazi nyingine tena ni kazi mojawapo nzuri sana. Wakulima ndio mnaotupatia chakula na kuilisha nchi. Hata Mungu kazi ya kwanza kumpa mwanadamu ilikuwa kilimo.

Sasa kwanini wakulima mnaichukulia kazi yenu kana kwamba sio kazi. Imefikia hatua hadi watoto wenu wakiulizwa "Baba yako anafanya kazi gani?" Watajibu "Hana kazi ni mkulima tu." Hii ni kwa sababu tu mmeifanya na kuiona kazi yenu kama kitu cha kawaida.

Kuna baadhi ya watu wameitambua kazi ya ukulima kama kazi. Watu kama wakina Jakaya Kikwete, Mizengo Pinda na Dada Hadija Jabiry. Hao wanatambua kwamba kilimo ni kazi na wamefanya mambo makubwa sana kwenye sekta ya kilimo.

Uzuri wa mkulima unapata majibu yako papo kwa papo. Unavuna ulichopanda na kuweza kupata chakula. Ninyi wakulima ndiyo mnafanya nchi iendelee kwani likitokea baa la njaa nchi nzima tutatafutana. Yaani nchi haitakalika. Ukitaka kuhakiki jambo hilo nenda katika nchi zenye ukame. Nchi zenye baa la njaa.

Wakulima jivunieni kazi yenu. Ukulima ni kazi kama zilivyo kazi zingine. Kuna watu wengi wametajirika kupitia sekta ya kilimo. Nitafurahi kusikia Leo mkijivunia kwamba kilimo ni kazi yenu. Watoto wenu pia muwafanye watembee vifua mbele wakijisifia kwamba ninyi wazazi wao ni wakulima. Leo hii watoto wenye wazazi wakulima wanaogopa kutaja kazi za wazazi wao wakiogopa watachekwa. Lakini hili mmelianzisha wazazi kwa kuona kilimo si kazi.

"Mafanikio yako mikononi mwako."

Ndimi:
 Edius Katamugora
Author and motivational speaker
0764145476
0625951842 (WhatsApp)
Email: ekatamugora@gmail.com

Jipatie kitabu cha Barabara Ya Mafanikio kwa shilingi 6000/= tu. Dar es Salaam, Morogoro, Kagera, Iringa, Mwanza tayari vinapatikana. Mikoani tunatuma pia. Mawasiliano; 0764145476/0625951842

Imani yangu mafanikio ni kitu cha kushirikishana. Mshirikishe pia na rafiki, ndugu au jamaa kile ulichojifunza.


Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: