Habari rafiki yangu? Bila shaka unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku. karibu katika siku nyingine ya makala za BIDEISM BLOG. Makala zitakazo kuhakikishia kusonga mbele kadiri unavyoweza ili kufikia ndoto zako.
Katika makala ya leo nitaongelea kitu kinachoitwa UOGA WA UPINZANI. Hii ni hali ya kushindwa kujiwekea mipango na kuiweka katika matendo, kwa sababu ya kufikri watu wengine watakufikiriaje, watafanyaje au watasemaje. Huyu ni adui mkubwa wa kupoteza nguvu za kutoendelea kufanya jambo Fulani, kwasababu linakuwa katika fikra za mtu husika, ambapo uwepo wake haujulikani.
Ebu tuangalie dalili za woga wa upinzani. Watu wengi
uruhusu ndugu wa karibu, marafiki, na jamii kwa ujumla kuwashawishi kwamba hawawezi kuishi maisha yao, kwasababu
ya uoga wa upinzani.
Watu wengi wanakosea kwenye ndoa, kushindwa kuchuuza na
kuishia maisha magumu na yasiyo na furaha, kwasababu wanawoga wa upinzani
inayoweza kufata kama wakisahii makosa yao. (mtu yeyoyote aliyepitia katika uoga huu anajua maumizi yaliyojitokeza, yameharibu mipango yake, kazi zake hata
ule moyo wa kufanikiwa).
Mamilioni ya watu wanakataa kurudi shule, baada ya kuacha
shule kwa sababu ya uoga wa upinzani. Kuna namba kubwa isiyyo hesabika ya watu
wanoogopa kujikita katika MAJUKUMU Fulani kwa sababu ya uoga wa upinzani. Watu
wanaogopa kujihusisha na biashara kwa sababu ya uoga wa upinzani. Katika hali
kama hizi woga wa upinzani ni kubwa kuliko ile hamu ya kufanikiwa.
Watu wengi hukataa kujiwekea malengo makubwa au hata
kupanga kazi watakazo kuja kuzifanya kwa sababu ya uoga wa upinzani kutoka kwa
‘’maraf iki’’ ambao wanaweza
kumwambia ‘’ Husiwe na malengo makubwa, watu watadhani umechanganyikiwa’’. Messi ambaye ni mcheza maaarufu duniani anasema ‘’ Niliuza chai
mitaani ili nipate pesa za kunisaidia kufanya mazoezi uwanjani’’ alifanya hivo
na hakujali watu wangesemaje kuhusu yeye. Leo hii nani asiyemfahamu Messi kwa
uhodari wake wa kusakata kabumbu safi uwanjani. Ni kwa sababu alilenga pakubwa
na hakusikiliza watu wanasemaje. Dunia imejaa wakatisha tama.
‘’ Ili ufanikiwe unahitaji kujifunza
kupambana na woga wa kukataliwa( fear of rejection), kitu ambacho nilijiambia
nafsini mwangu, ambacho wananifikilia sio biashara yangu. Kitu ambacho ni cha
muhimu ni ninachofikiria kuhusu mimi ‘’ alisema Robert Kiyosaki
mwandishi wa vitabu maarufu duniani.
Naye bwana Tony
Robbins alikuwa na haya ya kusema ‘’ siri ya mafanikio ni kujifunza kutumia
maumivu badala ya maumivu kukutumia wewe, ukifanya hivyo unayaongoza maisha
yako na usipofanya hivyo maisha yako yanakuongoza’’ . jitahidi uwaoneshe wale watu wanaokwambia
jambo Fulani aliwezekana kwamba linawezekana ( Prove them wrong).
Nimegundua kwa mawazo mengi bado yanazaliwa, na yanaitaji
pumzi ya maisha ambayo kwayo
yanahitaji kuwekwa katika mipango na kuwekwa katika utendaji wa haraka sana.
Muda wa kulilea wazo ni pale linapozaliwa. Kila linapoishi linapata muda zaidi
wa kukua. Woga wa upinzani umekuwa ni chanzo.kikubwa cha kuharibu mawazo ambayo
hayafikii kwenye mipango na utendaji. Jenga ndani yako moyo wa kuendele kufanya
kitu Fulani hata kama umekosa watu wa kukusadia (support). Baba wataifa Mwalimu
J.K.Nyelele aliwahi kusema ‘’it can be done, play your part)
akimaanisha inawezekana cheza nafasi yako.
Ni mimi rafiki na ndugu yenu.
EDIUS BIDE KATAMUGORA.
Tuwasiliane;
0764145476.
Whatsapp; 0625951842 ( tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu whatsapp)
email; ekatamugora@gmail.com
Endelea kusoma makala nzuri katika blog hii. ASANTE
''See you at the top''.
0 comments:
Post a Comment