Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vizuri kupambana kutimiza ndoto zako.
Karibu katikw mada ya Leo inayosema" mvua unyesha pote/kote".
Ivi katika maisha yako kuna sehemu uliwahi kusikia ambako mvua haifiki. Wengine watafikiria jangwani lakini nako mvua unyesha hata kama ni Mara moja kwa mwaka.
Katika maisha kuna watu ambao kila siku ya Mungu kitu kikubwa wanachokifanya ni kukimbia mvua wanasahau kwamba mvua inanyesha na huko wanakoelekea.
Kwanini nimechukua mfano wa mvua?. Mvua kwa mada hii ni sawa na matatizo. Kila mahali katika maisha yetu kuna matatizo.
Mwingine hana kazi Ilo ni tatizo lakini pia kuna wenye kazi ambao hawazifurahii kabisa wanafanya ili mradi siku ipite. Wanatamani wastaafu lakini waliostaafu pia hawanafuraha na maisha waliyonayo."mvua unyesha pote"
Mwingine aliyeajiriwa anatamani ajiajiri lakini kumbe walio jiajiri wana matatizo makubwa zaidi wanakumbana na Shida kubwa.
Bofya hapa kusoma: Ulipo ni mahali sahii
Hivyo jambo la kutambua ni kwamba kila mahali kuna matatizo, kukimbia matatizo sio suruhisho uwenda unakokimbilia ndiko kwenye rundo la matatizo zaidi ya ulikotoka. Unajikuta mtu mwenye kutoa lawama kila wakati.
Tufanye nini sasa?
Jambo la kutambua hapa kwanza ni kwamba mvua hunyesha kote ivyo hamna haja ya kuikimbia
Kitu ambacho kinapaswa kufanyika ni kukaa chini na kutafuta namna ya kutatua matatizo tuliyonayo na si kuyakimbia.
"Kukimbia matatizo ni sawa na kuyaongeza ni sawa na kujiua mwenyewe".
Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476.
0625951842 (tuma neno SUBSCRIBE niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
Email: ekatamugora@gmail.com
Facebook page; bideismblog
Usisite kuwashirikisha wenzako kile unachokipata hapa. Asante
"See you at the top".
0 comments:
Post a Comment