Thursday, 5 January 2017

Ulipo Ni Mahali Sahii

Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba u mzima wa Afya na unaendelea vizuri katika kupambana kuyatafuta mafanikio. Leo ni siku nyingine tena iliyojaa tunu kubwa ya mafanikio yako.

Hivi umewahi kuwaza Michael Jackson angekuwa mcheza mpira nini kingetokea?. Mawazo yangu Mimi yananipeleka na kusema kwamba angekuwa mtu wa kawaida yaani asingefanya vizuri kwenye mpira kama alivyofanya kwenye muziki. Hiki ndicho kilicho nisukuma kuandika makala hii "Ulipo ni mahali sahii".

Bofya hapa kusoma; je umejiandaa?

Kuna watu wengine, wamawaza labda wamezaliwa na wazazi wasio sahii, wengine wanawaza labda wanafanya kazi zisizo sahii, wengine wanafikiri shule au vyuo walivyopo sio sahii. Kuna wengine wanawaza na kudhani hata wapenzi walionao sio sahii. Leo nataka nikwambie ulipo ni mahali sahii.

Kuna hadithi moja ya mchimba madini uko Afrika, aliyekuwa na sehemu kubwa ya ardhi, alichimba bila kufanikiwa kupata hata kijiwe kidogo cha madini lakini wenzake maeneo mengine walipata madini mengi tu. Baada ya kuona hafanikiwi aliamua kuuza ile ardhi kwa bwana mwingine, na kwenda kununua ardhi sehemu nyingine ili apate madini. Bwana huyu mpya alichimba mita moja na kukuta bahari ya madini. Yule mmiliki wa kwanza kusikia hivyo aliamua kujiua.

Bofya hapa kusoma: Hiki ndicho kiwanda unachokimiliki wewe

Hadhithi hii inatufundisha kwamba tutafute kwanza kile kilicho bora katika mazingira tuliyopo. Kama unahisi wazazi wako sio sahii, tafuta kitu bora unachokiona ndani yao. Kama unahisi mpenzi wako sio sahii tafuta kitu bora unachokiona ndani take kabla ya kuamua mengine. Kama unahisi kazi yako sio sahii chunguza kwanza ubora wa kazi unayoifanya, ndio maana nasema ulipo ni mahali sahii.

Mkimbiaji namba moja duniani bwana Husen Bolt aliwahi kujaribu kucheza mpira wa miguu lakini hakufanikiwa kung'aa kama alivyo sasa kwenye mbio. Michael Jordan mchezaji maarufu wa kikapu duniani naye aliwahi kujaribu kucheza mpira wa gofu lakini alionekana mtu wa kawaida.

Je nifanyeje kujua nilipo kama ni sahii?.
Jambo la msingi kwanza hapa ni kupenda pale ulipo. Ukipenda kwa moyo wa dhati mahali ulipo utagundua ni mahali sahii kwako.

Jambo la pili ni kuongeza jitihada na kujitahidi kufanya kazi kwa bidii kufanya pale ulipo paonekane pazuri zaidi ya palivyokuwa mwanzo. Kuna msemo wa kiingereza unasema;

"Dig gold where you're" ukimaanisha chimba dhahabu mahali ulipo. Usitamani kwingine wakati mahali ulipo ndipo sahii. Usitamani kwingine wakati mahali ulipo ndipo penye barabara ya mafanikio.

Ni Mimi rafiki na ndugu yenu.
Edius Katamugora
Tuwasiliane;
0764145476.
Whatsapp; 0625951842 (tuma neno ''SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu)
Email: ekatamugora@gmail.com
Instagram; @eddybide
Facebook page: bideismblog

Usisite kuwashirikisha wenzako kile unachokipata hapa. Asante.

"See you at the top".

Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.

0 comments: