Habari mpendwa msomaji wa Bideism blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea kuweka juhudi kwenye kile unachokifanya.
Karibu katika makala ya Leo ili kujifunza kitu kipya kitakachokusaidia kufanikiwa katika maisha yako.
Hii ni kanuni hai wanayoitumia watu wengi waliofanikiwa. Kanuni ya kuorodhesha malengo yao. Kila unapokuwa na wazo au lengo andika wazo lako chini na liwekee ufafanuzi ili lionekane ni wazo hai.
Ukishaorodhesha wazo lako weka muda muafaka unaotaka wazo lako litimie na tarehe husika. Mfano Mimi naweza andika "Kufikia tarehe 29 mwezi wa 6 mwaka huu nitakuwa nimetoa Kitabu changu na kuanza kukiuza". Hilo ni wazo lililoandikwa chini.
Ukimaliza kuandika lengo lako chini hakikisha unaliweka lengo lako mahali ambapo unaliona kila siku ili likupe motisha ya kuona kila siku kuna kitu unadaiwa kufanya ili kufanikisha lengo lako. Kwa mfano kama unandoto ya kuwa na gari au nyumba ukisha andika weka ata picha ya kitu unachokita ukutani au sehemu kinapooneka kiasi kwamba kila siku ya Mungu unaiona picha ya lengo au wazo lako.
Watu wengi wana malengo mengi lakini hawayaandiki chini. Wanayabeba tu vichwani na mwisho yanapotea kama yamepigwa na kibunga.
Lengo lolote uanza kwa kukamilika baada ya kuanza kuandikwa chini.
Tunaweza kujifunza hata kutoka kwa serikali ambayo kila mwaka mwezi wa sita ujadili bajeti ambayo huwa ni ya mwaka mzima inayotumika kuanzia mwezi wa saba ambapo mwaka MPYA was serikali huanza. Huu ni mfano halisi wa kuandika malengo chini na kuyafafanua.
Kuna mtu aliwahi kusema " A dream written down becomes a "PLAN". A plan written down becomes a GLOAL. A goal put into action makes a dream come true".
Jifunze Leo kuandika malengo na mawazo yako itakusaidia kuyafikia mafanikio unayoyataka.
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora.
Tuwasiliane;
0764145476.
0625951842 (tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
Email: ekatamugora@gmail.com
Usisahae kulike page yetu ya Facebook: Bideismblog
"See you at the top".
Tangazo; Nimeandika Kitabu kinachoitwa "Baraba ra Ya Mafanikio" unaweza kuweka "oda" yako mapema. Usikubali kupitwa (bei itatajwa mbeleni).
0 comments:
Post a Comment