Habari mpendwa msomaji wa Bideism Blog. Ni matumaini yangu kwamba umeamka salama na unaendelea vizuri na maisha yako na unaweka juhudi katika kutimiza ndoto yako.
Karibu sana katika makala yetu ya Leo.
Jana kuna mtu alinionesha video ya mtoto Fulani aliyeulizwa na mwalimu wake kwamba anatamani kuwa nani?. Mtoto huyo bila woga aliamka na kusema anatamani awe "smartphone" (simu janja). Mtoto huyo alielezea jinsi wazazi wake wanavyotumia muda mwingi kuchati na hata kumsahau mtoto wao. Mama yake inafikia hatua anasahau kumpa chakula lakini hasaau kuweka simu yake chaji. Video hiyo sema ukweli iliniumiza sana na ndiyo maana nimesukumwa kuandika ujumbe huu.
Watu wengi Leo hii wapo kama wazazi wa huyo mtoto wa kike. Kila akiamka lazima aanzie Facebook, huko atalike na kukomenti picha zote, baadae instagram, na baadaye whatsapp unakuta ana makundi zaidi ya tisa humo anashinda anachati na simu janja yake. Ni bingwa wa kufowadi Meseji toka group moja kwenda jingine.
Hilo alitoshi ataendelea kufuatilia skendo za wasanii utazani ni mwandishi wa habari. Mara anafatilia "Wema Sepetu kaenda chadema,anaidai ccm mamilioni", anashinda anashangilia ushindi wa simba mitandaoni anamzidi hata mmiliki wa timu Moh Dewj. Kama humo kwenye kundi hilo jiulize unaelekea wapi?.
Kama umenunua cm ili upige picha uweke mitandaoni na watu waje kulike, fikiria umeweka picha na wote wakaandika maneno yao mabovu, utajifikiriaje?. Au ndo utaamka umenuna na kudai leo ni siku mbaya kwako?, hii ni kwa sababu umehirusu simu iyaendeshe maisha yako. Leo jifunze kutumia simu yako ikuletee manufaa.
Tafuta magroup ya Whatsapp yanayojadili kuhusu mafanikio na fursa mbalimbali. Unaweza kuingia kwenye mtandao kama YouTube na kutizama video za wahamasishaji mbalimbali na zitakufungua kiakili na kifikra na utakuwa si mtu wa kawaida.
Kama ni mfanyabiashara hakikisha unatumia mitandao ya kijamii kujitangaza na hakikisha watu wanajua unafanya nini kupitia mitandao ya kijamii. Mfano Mimi kuna sehemu nikipita utasikia wananiita "Bideism" hii ni kwasababu tu natumia simu yangu kutangaza kile ninachokifanya.
Leo pia simu inaweza kukusaidia kusoma Vitabu mbalimbali ambavyo pia vitakusaidia katika maendeleo binafsi. Unaweza pia kutumia simu yako kujifunza kupitia makala mbalimbali za blogu tofauti tofauti. Nikupongeze wewe unayesoma makala hii kwani simu yako inakusaidia kujifunza vitu muhimu vitakavyokusaidia katika maisha yako.
Zamani kidogo ulikuwa unahudhuri semina katika kumbi maalumu. Leo hii unaweza Fanya simu yako kuwa ukumbi mzuri tu wa kufanyia semina (online semina/webnar), hizi zinaweza kuwa za kijasiliamali au kuelimisha kuhusu mambo mbalimbali.
Jiulize leo,nitatumiaje simu yangu ya mkononi kuniendeleza,simu yangu itaniingiziaje pesa badala ya Mimi kuweka vocha kila siku na sipati chochote.
Kiukweli simu zetu za mkononi zinafaida nyingi lakini wengi wetu simu zimekuwa chanzo cha hasara kwani zinatumika kuwanufahisha wengine wakati zimetengenezwa kutunufahisha watumiaji.
"Tujifunze kukua na teknolojia na sio teknolojia ikue zaidi yetu sisi wanadamu."
Ni Mimi rafiki na ndugu yako.
Edius Bide Katamugora
Tuwasiliane:
0764145476
0625951842 (Tuma neno "SUBSCRIBE" niwe nakutumia makala zangu moja kwa moja).
E-mail; ekatamugora@gmail.com
Facebook page; bideismblog
"See you at the top".
Tangazo: Nimeandika Kitabu kinaitwa "Barabara ya Mafanikio", unaweza kuweka oda yako mapema ujipatie nakala yako pindi tu kitakapotoka.
0 comments:
Post a Comment