MATUSI ni maneno machafu ya kumuudhi mtu. THAWABU ni tuzo au zawadi au malipo mema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kutii amri zake.
Kwa kuangalia maana hizi za maneno kichwa chetu cha habari hii, tunaona kabisa kuwa ni maneno yanayojielezea vizuri.
Ukitumia jicho la kiimani juu ya neno 'tusi' utajikuta ukipata maana kubwa zaidi juu ya neno hili. kumtukana mtu si kumuudhi tu bali inakuwa zaidi ya kumuudhi. Ukiendelea kutafakari utaona kuwa 'tusi' ni kumdhalilisha mtu, kumharibia sifa yake na kumuumiza kisaikolojia.
Watu wengine hudhani 'tusi' ni neno la kukanya, kukosoa au kukemea makosa au maovu katika jamii kumbe ni kinyume na dhana hii. Mtu akikosea na wewe ukitumia 'tusi' kwa nia ya kumkosoa/kumrekebisha jua wazi kwamba humrekebishi bali ni kujiondolea heshima na kufanyia dharau kwa cheo au nafasi uliyonayo katika jamii. Pia huonesha ni kwa jinsi gani unamdharau au humthamini.
Huwa kuna msemo '' Tafakari kabla ya kutenda/kunena'' waingereza wanaingia ndani zaidi na kusema ''Easy is to speak without thinking. Difficult is to refrain the tongue''. watu hudhani msemo huu hahusiani na matendo ya kinywa hivyo hutoa maneno tu mdomoni bila hata kuyatafakari na kuangalia athari yake ukatika jamii. Chukulia mfano wa mwanmke na mtoto wake, mtoto anakosea unasikia anatoa neno linalohusiana na mama wa mtoto au maumbile ya mwanamke!!. Anasahau yakwamba yeye ndiye mama na pia ni mwanamke hivyo maneno yale yanamrudia yeye hii inatokana na kukosa kutafakari na kuruhusu midomo yetu kutamka maneno mabovu.
Hii ni kujidhalilisha na kujiondolea heshima na ni mfano mbaya kwani kutumia matusi mbele ya mtoto ni kumfanya kutumia matusi kwa sababu anakalili na kuona kama lugha ya kawaida kumbe sivyo. mwisho wa siku ukimkuta anatukana unaanza kumuukliza ''nani kakufundisha?'', unasahau kwamba kakusikia wewe. Tafakari kabla ya kunena itakusaidia kuepuka kuingia vikwazo kama hivi na hata kupoteza heshima yako katika jamii ya watu wanaokuzunguka. kama haufikirii thawabu ikungojayo basi fanya kwa kutunza au kulinda hadhi yako katika jamii. Jitafutie thawabu kwa kubajeti maneno yatokayo kinywani mwako. Tafakari neno unalotaka kabla ya kutamka. usipofanya hivo utashangaa unadharaulika hata kwa wanao.
Makala haya yameandikwa na EVANCE MUJUNI (0657923679)
Friday, 10 March 2017
Edius Katamugora
Hii ni blogu rasmi ya Edius Katamugora, hapa utajifunza maendeleo binafsi, utapata makala mbalimbali zinazohusu biashara, elimu, hamasa na maisha kwa ujumla. Karibu sana katika blogu hii.
0 comments:
Post a Comment